Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa akisalimiana na wanyeji wake mara baada ya kuwasili kutembelea ujenzi wa mradi wa barabara ya juu ( fly over) ya Chang’ombe Jijini Dar es Salaam ambapo alikagua ukamilishaji wa upande mmoja kama alivyotoa maelekezo hapo awali ifikapo leo iweze kutumika. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kutembelea ujenzi wa mradi wa barabara ya juu ( fly over) ya Chang’ombe Jijini Dar es Salaam ambapo alikagua ukamilishaji wa upande mmoja kama alivyotoa maelekezo hapo awali ifikapo leo iweze kutumika. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa barabara ya juu ( fly over) ya Chang’ombe Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abdi Issango akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa barabara ya juu ( fly over) ya Chang’ombe Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya magari yakiruhusiwa kupita katika upande mmoja wa fly over Chang’ombe Jijini Dar es Salaam mara baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa kukagua na kuruhusu barabara hiyo iweze kutumika.
Moja ya barabara ya Juu (fly over) ya Chang’ombe Jijini Dar es Salaam ambayo imekamilika na kuanza kutumika ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo ambalo limekuwa ni changamoto.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa leo Mei 30,2022 amekagua ujenzi wa mradi wa barabara ya juu (fly Over) ya Chang’ombe Jijini Dar es Salaam na kuweza kushuhudia upande mmoja barabara hiyo kuruhusu magari kupita ili kupunguza msongamano mkubwa barabani.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo, Waziri Mbarawa amesema Serikali imekuwa ikihakikisha inakamilisha ujenzi wa barabara za juu katiika maeneo mengi Jijini Dar es Salaam ili Watanzania wapate muda mrefu wa kwenda kufanya shughuli za maendeleo na tukifanya hivyo tunaamini kwamba uchumi wetu utakuwa kwa kasi zaidi.
“Dar es Salaam tumeanza utaratibu wa ujenzi wa Fly overs na miezi mitatu iliyopita tullikuja na tukawaambia wakandarasi, kazi haijamalizika kwa asilimia 100 lakini lile eneo ambalo tunaweza kulitumia tulitumie, tunalitumia au tulitumie kwasababu ya kupunguza msongamano, nikawaelekeza wakandarasi kwamba itakapofika tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu fly over ya upande mmoja hapa Chang’ombe iweze kufunguliwa”. Amesema Waziri Mbarawa.
Amesema Fly Over hiyo haijaisha kwa asilimia 100 itafunguliwa leo na mara baada ya barabara yote kumalizika watarudi tena kuweka rami laini na kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa ujumla ambapo kutawekwa na mataa.
Aidha amewataka wananchi ambao watatumia barabara hiyo hasa madereva waelewe usalama barabarani kwa kutumia taratibu za usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizo za lazima na kusababisha barabara kuanza kuvunjwa bila sababu yoyote.
“Watakaopata fursa wajue wanawajibu kama madereva kwamba barabara hii ni kwaajili ya watanzania wote na tunataka barabara hii idumu kwa muda mrefu, tungalisema tusubiri baada ya miezi sita ndo tuweze kufungua barabara yote lakini haina mantiki”. Amesema
Pamoja na hayo ametoa maelekezo kuwa ifikapo mwwezi Oktoba, 2022 baarabara ya upande wa pili iwweze kukamilika na kuweza kufunguliwa ili iweze kutumika ili watanzania waweze kutumia barabara hizo na kupunguza msongamano wa magari katikka eneo hilo ambalo limekuwa changamoto.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila amemhakikishia Mhe. Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni Awamu ya Pili ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka BRT2 utakamilika kwa ubora na kwa wakati.
“Tunatarajia barabara hii ikamilike ifikapo mwakani mwezi Machi ujenzi huu wa BRT II na tubategemea kwamba kwa ujenzi huu wa BRT II ambapo kutakuwa na matumizi ya Mabasi yaendayo haraka basi kutakuwa na kupungua kwa sehemu kubwa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam”. Amesema Mhandisi Mativila.
Nae Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abdi Issango amesema madera wanatakiwa kuzingatia usalama barabarani kwa kuhakikisha wanakwenda kwa mwendo uliosalama ili kupunguza ajali katika eneo hilo.
“Jeshi la Polisi tutasimamia kuhakikisha kwamba miundombinu hii inakuwa salama, inaokoa ajali lakini foleni zinakwisha, tunafahamu foleni zinasababisha gharama kubwa za uendeshaji, gari linasimama mua mrefu na kutumia mafuta mengi hivyo tukipunguza foleni tunaweza kusababisha uchumi wa nchi kukua”. Amesema ACP Issango.
Hata hivyo ACP Issango amewahimiza wakandarasi wa ujenzi huo wajitahidi kumalizia ili angalau malengo ya serikali ya kuhakikisha kwwamba eneo hilo linakuwa na fly over na Jiji kuweza kupendeza na ajali zinapungua pamojja na uchumi kukua.