Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka DART Dkt.Edwin Mhende akizungumza wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na serikali za mitaa (USEMI) ilipotembelea Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na serikali za mitaa (USEMI) wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa DART Mhandisi Fanuel Kalugendo akitoa maelezo huhusiana na miundombinu ya huduma za usafirishaji wa abiria katika jiji la Dar es Salaam.Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na serikali za mitaa (USEMI) wakiwa katika usafiri wa mabasi yaendayo haraka wakati kamati hiyo ilipotembelea Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na serikali za mitaa (USEMI) wakipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka DART Dkt.Edwin Mhende wakati wa ziara ya kamati katika Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na serikali za mitaa USEMI Mhe.Abdallah Chaurembo wakifurahi jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka DART Dkt.Edwin Mhende mara baada ya kumkabidhi zawadi ya kikombo kwa niaba ya Kamati nzima.
**************.
*Wajumbe wa Kamati wapongeza DART kwa ufanisi wa kazi, DART na UDART watakiwa kukutana na kamati hiyo kuwapa maelezo ya kina
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Wakala wa Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umesema kuwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kwa Barabara kuanzia Mbagala kuelekea Gerezani kuanza Machi 23.
Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka DART Dkt.Edwin Mhende wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na serikali za mitaa (USEMI) ilipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam kwa kuangalia mifumo mbalimbali ya Wakala huo.
Dkt.Mhede amesema wakala huo unajivunia mifumo ya ukusanyaji mapato ambapo imeongezeka kutoka sh.bilioni 1.8 hadi kufikia sh.bilioni Tatu kwa Mwezi.
Amesema mifimo hiyo imetengenezwa na wataalam ambao ni watanzania ambapo umesaidia kuokoa fedha ya serikali.
Aidha Dkt.Mhede amesema kuwa malengo ambayo wamejiwekea ni kuhakikisha wanakwenda kutoa huduma bora ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam ambayo itachochea na uchumi kukua.
Kamati hiyo baada ya kupata taarifa za DART imeiagiza DART na UDART kukutana na kamati hiyo na kuwapa maelezo ya kina pamoja na sheria ilioanzisha mradi huo ambapo ndipo wanaweza kushauri serikali kama kuna jambo la kufanya.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Abdallah Chaurembo ambaye ni Mbunge wa Mbagara amesema kuwa mradi huo uko vizuri na kushauri waendelee kuboresha baadhi ya kasoro.
Mjumbe wa Kamati na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta ameiopongeza DART kwa kazi nzuri wanayoifanya katika utoaji wa huduma ya usafiri katika jiji Dar es Salaam.
Nae Mjumbe wa Kamati hiyo Bi.Mwantum Haji amesema kuwa DART wanafanya kazi nzuri ambayo matokeo yake yanaonekana katika usimamizi wa maradi huo na kuongeza kuwa wanaupiga Mwingi.