Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akizungumza na waandishi wa habari leo hii ofisini kwake
*****************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wito umetolewa kwa waajiri wote wa sekta binafsi walioko Mkoani Mwanza kujitokeza kwaajili ya kuandikishwa wao kama waajiri kwenye mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) sanjari na wafanyakazi wao kuandikishwa kama wanachama.
Wito huo umetolewa leo Ijumatatu Mei 30, 2022 na Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelekea kwenye hafla ya usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari kanda ya ziwa unaotarajiwa kufanyika Juni 3,2022 katika ukumbi wa Rock City Mall.
Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria namba 50 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2018 ambapo NSSF imepewa jukumu la kuandikisha sekta isiyo rasmi ambayo ina makundi mbalimbali kwenye Jamii wakiwamo bodaboda,mama lishe,wavuvi,na vikundi vya wanawake.
Amesema gharama za kujiunga na Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) kwa watu ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi anatakiwa kuchangia kiwango kisicho pungua 20,000 na mafao yatatolewa kulingana na kiwango alichokuwa akichangia.
Ameeleza kuwa kunaumuhimu mkubwa sana wa watu kujiunga na mfuko wa hifadhi ya Jamii kwani ni zaidi ya akiba ambayo itawasaidia katika kutimiza ndoto zao.
Ameeleza huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo na wanachama wamekuwa wakinufaika nazo ni pamoja na fao la uzazi,fao la kifo.
Mwisho amekipongeza chama cha waandishi wa habari Mwanza (MPC) kwa namna wanavyoisaidia jamii kupata elimu ya mambo mbalimbali.