Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza leo Mei 30,2022 jijini Dodoma na Watumishi wa Umma Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akifafanua jambo kwa Watumishi wa Umma Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu iliyofanyika leo Mei 30,2022 jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu iliyofanyika leo Mei 30,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu iliyofanyika leo Mei 30,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu iliyofanyika leo Mei 30,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu iliyofanyika leo Mei 30,2022 jijini Dodoma.
Meya wa Jiji la Dodoma, Prof David Mwamfupe,akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu iliyofanyika leo Mei 30,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Dodoma Swamweli Malecela,akimpongeza Rais Samia wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu iliyofanyika leo Mei 30,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Watumishi wa Umma Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
…………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WATUMISHI wa Umma mkoa wa Dodoma wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha mishahara yao kwa asilimia 23.3, posho za safari na kujikimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
Akizungumza leo Mei 30,2022 jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Rais Samia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,amewataka watumishi wa umma kuongeza uwajibikaji katika maeneo yao ya kazi ili kulipa fadhira zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita.
RC Mtaka amesema kuwa haitakuwa busara kama juhidi zilizofanywa na serikali chini ya Rais Samia za kupandisha mishara, kuongeza posho za safari pamoja kulipa malimbikizo ya madeni kama zitashindwa kuleta matokeo katika utumishi wa umma.
“Mimi kwa niaba ya watumishi wa mkoa wa Dodoma tunaahidi leo kuwa tutaendelea kumpaushirikiano mweshimiwa Rais kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni na miongozo”amesema Mtaka
Aidha, amewataka watumishi kuacha kujihusisha na mambo yasiyokuwa na tija kama vile ulevi na anasa zisizokuwa na tija kwao.
Kwa wake Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo,amewataka watumishi kutumia kiasi kilichoongezwa kwenye mishara yao kubuni miradi itakayo waongezea kipato na kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa.
“Kumekuwa dhana ya kuwa watumishi wanaomba rushwa kutokana na kipato kidogo lakini kwa hili alilolifanya Rais mbadilike katika utumishi wenu na kubuni miradi badala ya kutumia vibaya fedha za miradi ya maendeleo”amesema Kibwengo
Naye Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Dodoma Swamweli Malecela,amempongeza Rais Samia kwa nyongeza ya mishara ya asilimia 23.3 ambayo wao wamekuwa wakilalamikia kwa muda mrefu.