Kamati ya amani ya viongozi wa dini wakutoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
*************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kamati ya ya amani ya Viongozi wa dini Mkoa wa Mwanza wametoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili katika uongozi wake.
Kamati hiyo imetoa pongezi hizo leo Mei 30,2022 wakati wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Victoria Palace ulioko Jijini Mwanza.
Charles Sekelwa ni Mwenyekiti mwenza wa kamati ya amani Mkoa wa Mwanza,amesema wameamua kujitokeza kumpongeza Rais kwasababu moja ya jukumu la viongozi
wa dini ni kukemea, kushauri,kutia moyo na kushukuru kwa Yale yote mazuri yanayofanywa na Rais.
“Tumekutana leo kwaajili ya kumtia moyo,kumpongeza, kumshukuru Rais wetu kwa kazi nzuri anazozifanya katika Taifa letu na tunaaamini ni njia bora ya kufanya azidi kuwa na hamasa ya kufanya kazi yake vizuri”, amesema Sekelwa
Ameeleza kuwa uongozi wake umekuwa rafiki sana katika nyanja mbalimbali ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari, watumishi kupandishiwa mishahara jambo ambalo linachochea utendaji kazi wenye tija katika Taifa.
Kwaupande wake Shekh Hassan Kabeke ambae pia ni Mwenyekiti mwenza wa kamati ya amani Mkoa wa Mwanza, ameeleza kuwa Rais Samia ameweza kusimamia amani na utulivu wa nchi hali ambayo imesaidia watanzania kuendelea kufanya kazi zao za kujipatia kipato kwa usalama.
“Tunamshukuru na kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo anazidi kuilinda tunu ya amani tuliyopewa na mwenyezi Mungu, tunazidi kumuombea ili azidi kufanya kazi zake akiwa na hofu ya Mungu”,amesema
Jacob Mutash ni mchungaji wa Kanisa la E.A.G.T lilipo Kiloleli Jijini Mwanza, pia ni mjumbe wa kamati ya amani Mkoani hapa amesema amefurahishwa sana na uongozi wa Rais Samia kwani amekuwa kiongozi wa kipekee ambae anakutana na makundi mbalimbali katika Jamii ambayo ni wazee,viongozi wa dini,wanawake,vijana, wafanyabiashara sanjari na kutimiza,kutatua masuala kadhaa yaliyokuwa hakiwakabili.
Amesema kuwa mafanikio mengi yameonekana katika kipindi cha uongozi wake ikiwemo kujenga uhusiano na mataifa mengine hali itakayosaidia uchumi wa nchi kuzidi kuimarika.
Naye Sikitu Abubakar mjumbe wa kamati hiyo amesema kuwa Rais Samia amewaheshimisha wanawake na kuwafanya wazidi kuaminika kuanzia ngazi ya familia,Jamii na Taifa kwa ujumla kutokana na uongozi wake uliotukuka.