Na Mwamvua Mwinyi, MAFIA
Mkuu wa mkoa wa Pwani , Abubakari Kunenge ametoa Rai kwa wananchi waliovamia na kuweka kambi za uvuvi katika kisiwa cha NYORORO ,wilaya ya MAFIA kutii agizo la serikali kuhama mara moja katika kisiwa hicho .
Rai hiyo imekuja kutokana na kisiwa hicho kuwa ni eneo tengefu kwa ajili ya mazalia ya samaki katika bahari ya Hindi na sio vinginevyo.
Kunenge alitoa rai hiyo wakati alipofanya ziara ya Kikazi katika kisiwa hicho kukutana na wananchi hao ambao wamevamia kisiwa hicho ambacho hakina huduma za kijamii na kuanzisha makambi ya kudumu.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, serikali kupitia kwa Waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki tayari imeshakutana na wananchi na kuagiza waondoke katika eneo hilo.
“Lakini bado wameendelea kuwepo wanakaidi jambo ambalo limemlazimisha katibu mkuu wa wizara hiyo kutoa maelekezo mengine kwa uongozi wa mkoa akiutaka uongozi huo usimamie agizo la kuondolewa kwa watu hao”;!
Amewataka wananchi hao kuheshimu agizo hilo kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na hakuna mtu yoyote aliyeko juu ya sheria,
Vilevile aliwaasa, wananchi hao kupitia kwa mwenyekiti SAIDI LIKUWA kuunda kamati ya watu watano wafike ofisini kwake ili kujadiliana namna ambavyo wataweza kumaliza tatizo hilo kwakuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani ni sikivu na ina wajali wananchi wake.
Kwa upande baadhi ya wakazi hao wameiomba serilali kuhalalisha kisiwa hicho kuwa makazi ya watu na kuanzisha kitongopji ndani ya kisiwa hicho ili wananchi waweze kupata huduma za kijamii .