MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ametinga kwenye Kambi ya Coastal Union huko eneo la Mbauda Jijini Arusha akiwataka Wachezaji kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Azam FC hatua ambayo itawawezesha kucheza fainali na Dar Young African.
Leo uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha miamba miwili Coastal ‘Wagosi wa Kaya’ wanaminyana na Azam FC katika mchezo wa Kombe la Azam.
Wakati akizungumza na wachezaji wa Coastal, Malima alisema timu hiyo ina kila sababu kuwafunga Azam kwani hiyo siyo tishio kwao huku akitumia fursa hiyo akiahidi wachezaji kuwapa donge nono watakaposhinda mchezo huo.
Kapteni wa Coastal Amani Kyata alimuahidi Malima kwamba wachezaji wako katika hali nzuri huku wakiwa na ari ya ushindi wanachoomba ni dua tu.