NA MWANDISHI WETU, TANGA
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika maonesho ya
bishara na utalii kwa kutoa elimu kwa wanachama kupitia maonesho yanayofanyika
katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga.
PSSSF inashiriki katika maonesho haya pamoja na
kutoa elimu kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda hilo, pia wanachama
wanapatiwa huduma mbalimbali za kiofisi ikiwemo, kuangalia taarifa za michango ya wanachama, taarifa za malipo ya pensheni, uhakiki wa
wanachama na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya uanachama, alisema Bi. Rehema Mkamba, Afisa Mkuu wa Uhusiano, PSSSF
Alisema ni fursa nzuri kwa Mfuko kukutana na wanachama wake lakini wananchi pia ambao watafika kwenye maonesho hayo maarufu kama Tanga
Trade Fair ambayo yatadumu kwa siku 10 kuanzia Mei 28
hadi Juni 6, 2022.