Adeladius Makwega-DODOMA
Wakristo wakatoliki wameambiwa kuwa pale panapokuwepo na zuio au kutengwa kwa muumini yoyote ndani ya kanisa hilo kusudio si ubaguzi bali shabaha yake ni kulinda imani na msingi ya Kanisa Katoliki.
Kauli hiyo imetolewa Katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Mei 29, 2022 katika misa ya jumapili na muhubiri Damian Ndimbo Mjumbe wa Kamati ya Uinjilishaji kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
“Mnapaswa kuijua imani Katoliki, mmesikia wakatoliki wenzetu Iringa wamefungiwa kupokea sakramenti. Walienda kwenye kongamano la muhubiri maarufu Bulidoza wakajaa kule, walivyorudi mapadri wa pale manispaa wamewafungia sakramenti waumini wote waliokwenda huko, lengo lao zuri tu. Tunatafautiana aina za malisho, aina za vyakula, na malezi. Sisi ni wakatoliki, tuna mambo yetu, tuna watu wetu wenye karama na upako, kama una shida ya maombezi wapo Karismatiki Katoliki, wapo walei wanatoa huduma hizo, wapo mapadri wanatoa huduma hizo. Kuondoa michanganyo michanganyo ile, wamewafungia sakramenti.”
Pia muhubiri huyo alisisitiza kuwa kama mkatoliki ataishika imani yake vizuri hata akiwa kiongozi iwe kanisani au kiongozi katika vyama vya siasa na serikalini lazima atakuwa kiongozi wa mfano.
Muhubiri huyo alihitimisha mahubiri yake kwa kuzitaja changamoto kadhaa za maisha ya ndoa za sasa zikiwamo ndoa za mseto ndani ya kanisa hilo ambapo mkatoliki anapewa ruhusa kwa kibali maalumu cha kufunga ndoa na yule asiye mkatoliki.
Mahubiri hayo ambayo yalianza na utangulizi uliotolewa na Padri Paul Mapalala ambaye ndiye Paroko wa Parokia ya Chamwino Ikulu yaliweka wazi baraka zote za Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma na Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa muhubiri huyo kuhubiri kanisani hapo.
Kwa desturi za Kanisa Katoliki ni mara chache mno katika misa zake akiwepo Padri kumpa nafasi ya kuhubiri muumini ambaye siye mtawa kufanya hivyo. Hilo hufanyika kwa kibali maalumu