NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
IMEELEZWA kwamba mfumo wa Ni Konekt App utakuwa ndio mwarobaini wa kukomesha vishoka kwa sababu mfumo huo ni mteja mwenyewe anaunganishwa na Shirika la Umeme nchini Tanesco moja kwa moja.
Hayo yalisemwa na Afisa Uhusiano na Wateja wa Tanesco Mkoa wa Tanga Amon Michael wakati wa mkutano wake na Wakandarasi,Mafundi na Wadau wa Tanesco kuhusu kuutambulisha mfumo wa Nikonekt.
Pamoja na hilo lakini pia kuwaeleza uhusiano kati ya Tanesco ,Mkandarasi na Mteja ,Miiko yao ikiwemo kutoa wito kwa wakandarasi katika kutekeleza maboresho ya utoaji wa huduma ya Nikonect.
Alisema kwa sababu kupitia mfumo huo mteja mwenyewe anaunganishwa na Tanesco moja kwa moja hakutakuwa tena kuhitaji msaada hivyo anatakuwa anamchagua mkandarasi anayemtaka.
Aidha alisema pia wametoa mafunzo hayo lengo ni ni kuwaonyesha njia ambazo mteja anaweza kupata fomu ya awali kupitia mfumo huo mpya wa Ni Konect ili kuweza kuhakikisha wanapata huduma hiyo muhimu.
“tumekubalina na wakandarasi wenyewe watahakikisha wanafanya kazi kulingana na taratibu na sheria zilivyo bila kuathiri wateja wetu na wamehaidi kufanya kazi zao kwa waledi”Alisema
“Lakini pia wamelipongeza shirika hilo kwa kuanzisha mfumo wa kisasa ambao utaondoa urasimu kwa mteja,Tanesco na mkandarasi faida kubwa ikiwa ni kumrahisishia mteja na kumondolea usumbufu”Alisema
Hata hivyo alisema kwa wale ambao watapata huduma kupitia Nikonect watapata huduma kwa siku tatu na kila hatua inayofanyika anapokuwa akienda kupata huduma watapata taarifa huku akieleza wakijua kampuni zao zinafanya biashara ya kuuza fomu watamfanyia upelelezi na wakibainika watatoa taarifa kwa Uwura waweze kukufutia leseni,
Awali wakizungmza mara baada y mkutano huo Mariam Sangali ambaye ni Mwakilishi wa Kampuni ya Muya Express Electrical Contract kutoka wilaya ya Kilindi alisema mfumo huo ni mzuri kwa sababu unapunguza watu wa tanesco kukusanya fomu mtaani.
Mariam aliliomba Shirika hilo kuendelea kuboresha zaidi mfumo huo kutokana na kwamba unaonekana utakuwa ni mwarobaini wa kuondokana na tatizo la vishoka.
Naye kwa upande wake Furaha Shooo alisemamfumo huo walokuja nao shirika hilo utakuwa ni dawa ya kuwasaidia kutokomza vitendo vya vishoka mfumo wa Nikonekt ni mzuri sana.
“Mfumo wa Nikonekt ni mzuri na mmeningia Kidigitali lakini kubwa nimpongeza Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania kutokana na kazi kubwa wanayoifanya”Alisema
Hata hivyo Mkandarasi Mzee Awadhi Salmini alisema mfumo huo mpya utakuwa ni uzidhibiti tosha wa tatizo la vishoka na utatusaidia sana wananchi .