Katibu mkuu wizara ya Afya Prof Abel Makubi akiwa juu ya jengo la mama na mtoto linaloendelea kujengwa kwa gaharama ya shilingi bilion 3 katika hospitali ya mkoa wa Tabora kitete
Katibu mkuu wizara ya Afya Prof Abel Makubi akizungumza na watumishi wa Afya mkoani Tabora
***********************
Na Lucas Raphael,Tabora
Katibu mkuu wizara ya Afya Prof Abel Makubi amesema kwamba miundombinu isiyokuwa rafiki kwa wasichana/wanawake wakati wa hedhi zao ina athari kiafya wanaweza kupata maambukizi katika njia ya mkojo nakuweza kusambaa zaidi na kupelekea maambukizi kwenye mji wa uzazi na hatari ya kupata ugumba.
Alitoa kauli hiyo imetolewa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na maafisa wa afya kutoka wilaya zote za mkoa huo katika mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora .
Prof Makubi alisema kwamba kitendo cha hedhi salama akipiwi nafasi kubwa kutoka kwa jamii inayotunzunguka na hivyo wanawake wanashindwa kupata watoto kutokana na tatizo la hedhi kutokuwa salama
Alisema kwamba kuna baadhi ya jamii zina imani potofu kiasi cha kuwanyanyapaa wanawake na hivyo kuwa ngumu kuweka mipango ya maendeleo ya kuboresha usafi na hedhi salama hapa nchini.
‘’Jamii nyingi zinahusisha hedhi na uchafu au najisi. Hali kadhalika, maumivu ya tumbo wakati wa hedhi uhisiwa kuwa msichana au mwanamke ametoa mimba au amejamiana na mume wa mtu mwingine au anadanganya/anajisingizia’’alisema Prof Makubi
Alisema kwamba wanawake ama wasichana wengi huwa wanapata changamoto ya kutomudu gharama za taulo za kike, kupata maji salama na pamoja na vyoo bora.
Katibu huyo mkuu wa wizara ya Afya alisema kwamba jamii inapaswa kutambua kuwa hedhi salama ni afya na ni baraka za uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
Prof Makubi alisema Wizara itaendelea kutoa elimu ya Hedhi Salama kwa jamii kwa lengo la kuhamasisha, kuvunja ukimya na kuachana na mila/desturi potofu kuhusu hedhi
Aidha, alisema kwamba watahakikisha kuwa Sera ya Afya inaliweka jambo la hedhi salama kuwa moja ya vipaumbele vyake ili kutunza heshima na utu wa mwanamke na kumpa nafasi ya kuleta maendeleo katika jamii.
Hedhi Salama ni msichana/mwanamke anapokuwa katika siku zake anatakiwa kuwa katika mazingira salama ambapo anapata huduma zote muhimu ikiwemo miundombinu ya vyoo vyenye usiri, maji safi, taulo za kike au vifaa salama vya kujisitiri na utupaji salama wa vifaa/taulo za kike zilizotumika.