********************
26/05/2022 TABORA
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameitaka jamii kuachana na vitendo vya wizi wa mifungo na kwamba Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu hao ili kukomesha vitendo hivyo.
IGP Sirro amesema hayo wakati akizungumza na Watendaji na Wenyeviti wa serikali za Mitaa pamoja na wananchi wa mkoa wa Tabora ambapo amewataka wananchi kuendelea kutimiza wajibu wao katika suala la ulinzi na usalama kwenye maeneo yao ili kuhakikisha kuwa hakuna mhalifu anayepata nafasi ya kutekeleza uhalifu.
Naye mmoja kati ya Wenyeviti wa serikali za mtaa Bwana Rashid Hamad ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Subira Kata ya Chemchem mkoani Tabora akizungumza kwenye kikao hicho amesema kuwa, katika mtaa wake kumekuwa na changamoto nyingi hasa zinazotokana na waendesha pikipiki maarufu bodaboda kwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwenye mtaa anaouongoza.