Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,Hargeney Chitukulo akisaini kitabu hicho Leo baada ya kukaimishwa nafasi hiyo jijini Arusha.
……………………………………………
Happy Lazaro,Arusha.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha,Dk, Athumani Kihamia ametoa tahadhari kwa baadhi ya watumishi wa Jiji la Arusha kuacha mara moja kuwavunja moyo watumishi wengine baada ya kusimamishwa kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima.
Kihamia ameyasema hayo leo Mei 26 jijini Arusha wakati alipokuwa akitekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilotoa juzi mara baada ya Dk,Pima kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi na kuongeza kuwa Sektretarieti ya Mkoa wa Arusha imemteua Hargeney Chitukulo kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha hadi hapo mamlaka husika zitakapoamua badae.
Chitukulo ambaye alikuwa ni Katibu Tawala Msaidizi,Mchumi na Uzalishaji Mali Mkoa wa Arusha amechukua nafasi hiyo baada ya Pima kusimamishwa kazi na wenzake watano ambao ni Nuru Sarakwa,Mariam Shabani , Innocent Mduhu,Alex Daniel,Joel Mtango
Amesema baadhi ya watumishi wa Jiji wamekua na tabia ya kuwavunja wenzao mioyo ya kufanya kazi kwa madai ya kuwatisha kuwa nao watachunguzwa
” Tuhuma ni tuhuma tu hivyo zinachunguza na naomba mumpe ushirikiano Kaimu Mkurugenzi Chutukulo na asiyempa ushirikiano atachukuliwa hatua za kinidhamu”amesema Kihamia.
Amesema kuwa, uchunguzi huu ni wa ukaguzi maalum na timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ndio wanaokagua huku zile timu nyingine za Tamisemi,Mkaguzi wa Ndani zikiwa zimeacha kufanya hiyo kazi
Ametoa rai kwa watumishi kumpa ushirikiano Chitukulo ambaye ndiye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo kwa Sasa.
“Kuanzia leo Chitukulo ndiye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji kwa sasa na atakayeenda kinyume na maagizo ya Mkurugenzi huyo atachukuliwa hatua.
Naye Kaimu Mkurugenzi, Chutukulo aliiomba ushirikiano baina yake na watumishi hao katika kutekeleza majukumu yake
“Naomba ushirikiano ngazi ya Mkoa hadi wilaya na watumishi wengine pia”
Naye Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iraghe alimkaribisha Chitukulo na kumhakikishia kushirikiana naye katika kutimiza majukumu ya serikali.
Chitukulo amechukua nafasi ya Pima baada ya Waziri Mkuu kumsimamisha kazi kwaajili ya kupisha uchunguzi kutokana na ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka.