Dkt. Hedwiga Swai(aliyesimama) Mwenyekiti wa Kamisheni wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS)akisalimia wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa KUdhibiti UKIMWI (ATF) na Kamisheni wakati wa kikao cha Pamoja chenye lengo la kufahamiana na kujadili shughuli mbalimbali zinaotekelezwa na TACAIDS, kikao hicho kilichofanyika tarehe 25 Mei,2022 jijini Dodoma,kulia kwake ni Bibi Caroline Mdundo Mwenyekiti wa Bodi ya ATF na kushoto kwake ni Dkt Leonard Maboko Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS.
Dkt Leonard Maboko Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS akifafanua lengo la TACAIDS kukutanisha bodi hizo mbili, Bodi ya ATF na Kamisheni ambazo zote zinaisimamia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma Tarehe 25Mei,2022.
Wajumbe wa Kamisheni,wajumbe wa Bodi ya ATF na Menejimenti walioshiriki kikao cha pamoja kwa lengo la kufahamiana pamoja na kujadili majukumu ya Bodi zote mbili,majukmu ya TACAIDS , muundo na tathimini ya utekelezaji wa Mkakati wa nne (MNSF IV) , Vipaumbele vya Mkakati wa tano wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania(NMSF V) na matokeo yanayotegemewa pamoja na mpango wa utekelezaji wa ATF na Mapendekezo ya kuboresha vyanzo vya fedha vya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI.
Bw. Richard Ngirwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango akiwasilisha tathimini ya utekelezaji wa Mkakati wa nne (MNSF IV) ,vipaumbele vya Mkakati wa tano wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania(NMSF V) na matokeo yanayotegemewa katika kikao cha Kamisheni na bodi ya ATF kilichofanyika tarehe 25Mei,2022 Jijini Dodoma.
Dkt. Sajida Kimambo Mjumbe wa Kamisheni ya TACAIDS akizungumzia umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa huduma za kutokomeza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kutoka kushoto ni Prof.Magreth Bushesha na kulia kwake ni Bibi Bahati Haule. Wote ni makamishina wa tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania.Bibi Caroline Mdundo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI akijadili ajenda ya muundo wa TACAIDS baada ya kuwasilishwa na wataalam, wakati wa majadiliano katika kikao hicho kilichokutanisha bodi ya ATF na Kamisheni Tarehe 25 Mei,2022 Jijini Dodoma.