**************************
Na Silvia Mchuruza,
Bukoba,KAGERA.
Uongozi wa shule ya msingi rubale iliyopo halmashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini mkoani KAGERA umeiomba serikali na wadau wengine kusaidia ujenzi wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi went ulemavu katika shule hiyo.
Lengo likiwa Ni kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu ambayo husababisha kushindwa kumaliza masomo yao .
Ombi Hilo limetolewa na mkuu wa shule hiyo Leodigard Lucas wakati shirika la world vision Tanzania Kanda ya KAGERA likikabibidhi kwa serikali vyumba vinne vya madaras matundu 12 ya vyoo na mifumo ya kunawia mikono tangi la kuvunia maji ya mvua na madawati 400 vilivyofadhiliwa na shirikala Hilo kupitia mradi wa Rukoma AP.
Mwalimu Lukasi amesema kuwa katika shule yake wapo Watoto 26 wenye ulemavu wa aina tofauti wanaosoma katika kitengo maalumu na kwamba uwepo wa mabweni utawezesha hata wanafunzi wenye ulemavu walioshindwa kuwaandikishwa shule kutokana na umbali kupata fursa ya kusoma.
Naye mkuu wa idara ya elimu msingi katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba Gregrol Fabian amesema kuwa serikali inatambua uwepo wa Watoto wengi wenye uhitaji maalumu ambao hawajapata fursa ya kusoma kutokana na ulemavu walio nao na kwamba wanaendelea na mazungumzo na wadau likiwamo shilika Hilo ili kujengewa mabbweni katika shule maalumu za Rubale na Ryamaoro A.