Dkt Hedwiga Swai (aliyesimama)Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) akizungumza na watumshi wa TACAIDS wakati wa hafla ya kugawa vyeti na zawadi kwa wafanyakazi Hodari wa mwaka 2021 tarehe 24Mei,2022 Jijini Dodoma,pembeni yake ni CPA (T) Magreth Mrema,Mwenyekiti wa tawi- TUGHE TACAIDS.
Dkt Leonard Maboko(aliyesimama) Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS akitoa ufafanuzi kwa Kamisheni kuhusu umuhimu wa chama cha wafanyakazi TUGHE kwa Kamisheni,kulia kwake ni Bw.Samuel Nyungwa,Katibu TUGHE Mkoa wa Dodoma na aliyekaa kulia ni Mwenyekiti wa Kamisheni wa TACAIDS Dkt Hedwiga Swai.
Samuel Nyungwa,Katibu TUGHE Mkoa wa Dodoma akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya kudhibiti UKIMWI TACAIDS wakati wa hafla ya kugawa vyeti na zawadi kwa wafanyakazi hodari wa mwaka 2022 jijini Dodoma.
CPA(T) Bw.Karison Konga,(aliyeshika cheti) ambaye ni Mfanyakazi bora wa TACAIDS wa mwaka 2021 wa kwanza kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya TACAIDS Dkt Hedwiga Swai, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Leonard Maboko. Kulia ni Bw. Bw.Samuel Nyungwa,Katibu TUGHE Mkoa wa Dodoma akifuatiwa na CP(T) Magreth Mrema Mwenyekiti wa Tawai la TUGHE –TACAIDS.
Baadhi ya watuishi wa TACAIDS wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamisheni wa TACAIDS pamoja na wafanyakazi hodari kutoka katika Idara na Vitengo vya Tume ya KUdhibiti UKIMWI Tanzania.
Wajumbe wa Makamishina, Menejiment wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi hodari wa Tume wa mwaka 2021.
Dkt Hedwiga Swai Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI TACAIDS akifungua kikao cha 49 cha Kamisheni hiyo kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 24Mei,2022
Dkt Leonard Maboko Katibu wa Kamisheni wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI TACAIDS akifafanua moja ya hoja za katika kikao hicho kilichofanyika Tarehe 24Mei,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamisheni wakifatilia kikao cha Kamisheni cha 49 cha Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) kilichofanyika tarehe 24Mei,2022 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TACAIDS Bw. Yasin Abas akifafanua hoja kwa kamisheni wakati wa kikao cha Kamisheni kilichofanyika jijini Dodoma Mei2022
Baadhi ya wajumbe wa Menejiment kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) wakifatilia ufafanuzi kutoka meza kuu katika hoja zilizowasilishwa wakati wa kikao cha Kamisheni kilichofanyika tarehe 24Mei,2022 jijini Dodoma.
****************
Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania imepongezwa kwa kufanya kazi nzuri na kutekeleza majukumu kwa kufuata utaratibu na kanuni zilizowekwa katika mipango yake ya utekelezaji wa shuhghuli za Tume.
Akifungua kikao cha 49 Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS),Dkt Hedwiga Swai,amesema kuwa pamoja na mambo mengine lakini anaanza kwa kuwapongeza TACAIDS kwa kazi nzuri wanayoifanya katika utekelezaji wa majukumu ya tume.
“Nawapongeza kwa utekelezaji wa shughuli zenu kwa kufuata utaratibu na kanuni,hongereni sana, nimepata taarifa kuwa mmepata hati safi ya ukaguzi wa CAG kwani sio jambo dogo lakini naomba mwendelee kufanya hivyo msije sifiwa baada mkarudi nyuma.hongera sana DKt Maboko na timu yako kwa ujumla”.alisema Dkt Hedwiga.
Dkt Hedwiga amesema amefurahishwa na jinsi ambavyo Tume imeendelea kufatilia madeni ya wafanyakazi na waliowengi wamelipwa madeni yao,jambo linaleta amani kwa watumishi kwani mtu akipata haki yake kunakuwa hakuna manung’uniko.
Naye mjumbe wa Kamisheni hiyo Bw.Peter Maduki ameitaka tume kuhakikisha inaboresha uandishi wa taarifa kwa kuhakikisha kuwa taarifa ziwe na takwimu, Mafanikio na changamoto zinazojitokeza ili kamisheni ione namna ya kutoa mchango wake.
Kikao cha Kamisheni kinafanyika kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania Na. 22 ya mwaka 2001 na marekebisho yake Na.6 ya mwaka 2015 kikiwa na lengo la kufatilia utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS katika Mwitikio wa Taifa.
Baada ya kikao hicho Mwenyekiti alipata nafasi ya kukutana na baadhi ya watumishi wa Tume pamoja na wafanyakazi hodari na kuwatunuku vyeti pamoja na zawadi,ambapo mfanyakazi hodari wa jumla kutoka TACAIDS ni Mhasibu Mkuu CPA(T) Karlson Konga.
Akiwakabidhi vyeti hivyo Dkt Hedwiga amewataka wafanyakazi wa TACAIDS kudumisha umoja na ushirikiano kwani ni kitu muhimu sana katika utekelezaji wa majumu yao.