**********************
Na Silvia Mchuruza,
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Moses Machali amewaaagiza viongozi wa Jumuiya za maji vijijini CBWSO kuwahamasisha wananchi kutumia maji ya mabomba ambayo Ni miradi iliyojengwa na serikali na kuachana na utumiaji wa maji ya mitoni.
Agizo hilo amelitoa katika kikao Cha wadau wa maji kilichofanyika katika ukumbi wa chemba wilaya ya Bukoba mkoani kagera ambapo amesema Hadi sasa utumiaji wa maji ya bomba vijijini katika wilaya ya Bukoba ni asilimia 74.1 Jambo ambaro bado lengo la serikali alijatimia.
“Serikali inatarajia kufikia mwaka 2025 utumiaji wa maji iwe Ni asilimia 95 mjini na asilimia 85 vijijini kwaiyo inabidi viongozi kutoa uhamasishaji kwa wananchi ili kufikia lengo la serikali maana kwa sasa utumiaji wa maji ya bombani kwa wilaya ya Bukoba Ni asilimia 74.1”
Aidha DC machali amesema kuwa atowafungia macho wale viongozi ambao wana tumia nafasi zao kuwazuia wananchi kutotumia maji ya bombani kwa kisingizio Cha kuwepo kwa maji ya mitoni.
Hata hivyo nae meneja wa maji Ruwasa wilaya ya Bukoba eng. Evaristo Mgaya amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali bado Ruwasa inatekereza miradi ukiwemo mradi wa maji katika Kijiji Cha kashenge na irogero na miradi hiyo inagalimu kiasi Cha zaidi ya million 739 kutokana na fedha za UVICO 19 zilizotolewa Rais.