**************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, ametembelea Mradi wa barabara ya kiwango cha Zege Kwala-Vigwaza inayounganisha katika mradi mkubwa wa Kimkakati wa Bandari kavu Kwala yenye urefu wa km.15.5 ambao utagharimu sh.bilioni 36 na umefikia asilimia 54.1.
Barabara hii inapunguza athari zitokanazo na kupitisha malori mazito kwenye barabara ambazo hupelekea matengenezo ya barabara kuwa na gharama kubwa kila wakati,ni mkombozi kwa vijiji vya Vigwaza,Mnindi na Kwala na itarahisisha shughuli za uchukuzi kati ya bandari na barabara Kuu ya Morogoro.
Akitembelea mradi huo pamoja na kujionea Hali ya ujenzi bandari kavu ya Kwala , Kunenge alieleza ,Ni ziara inayojibu maelekezo waliyopewa na Katibu kiongozi wiki kadhaa zilizopita wakati alipofika eneo hilo na kuwataka kuhakikisha ndani ya miezi mitatu barabara na bandari hiyo iwe imeanza kazi.
“Mradi huu unakwenda katika maeneo makubwa ya uwekezaji Kongani ambayo itajengwa viwanda 300-350 ,Bandari Kavu, maeneo ya kubadilisha vichwa vya treni”:
“Tunampongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan,aliahidi kutekeleza na kumaliza miradi iliyoanza tangu kipindi cha awamu ya tano na kuanzisha miradi mipya Kama huo wa Kongani ya uwekezaji wa viwanda”:alisema Kunenge.
Kunenge alielekeza ,miezi mitatu barabara ya zege na bandari iwe imekamilika na kuanza kutoa huduma.:;”- ,Lakini tunafahamu pia itaendelezwa kujengwa barabara nyingine ya njia mbili “:Kazi yetu Ni kusimamia na kuhakikisha miradi hii inajengwa kwa viwango vinavyotakiwa na kukamilika kwa wakati kwa manufaa ya wananchi na Taifa.”
“Ni eneo la kimkakati, wenzetu wa Burundi,Uganda,Rwanda watakuwa na eneo la kuhifadhi mizigo Yao ,Ni eneo linalozunguka viwanda watakuwa wanasafirisha mizigo Yao,tutakuwa na reli SGR, barabara, EPZA.”
Mkuu huyo wa mkoa alibainisha wapo nyuma ya Rais kusimamia miradi yote ,na eneo la uwekezaji ambapo ametembea falme za Kiarabu,Dubai,Ufaransa, Marekani kutafuta wawekezaji na kuitangaza nchi matarajio yetu kupata wawekezaji wengi na mkoa upo vizuri .
Awali msimamizi wa mradi wa barabara hiyo, Jacob Mambo alisema , mradi ulianza Novemba 2020, Mamlaka ya Bandari (TPA) ilimpatia Wakala wa barabara Tanzania TANROADS jukumu la kusimamia ujenzi wa barabara hii Kama Mhandisi Mshauri kupitia kitengo Cha TECU Mkoa wa Pwani.
Alifafanua, matabaka ya chini yameshafikia zaidi ya asilimia 90 ya kazi,Tabaka lililoimarishwa kwa saruji limejengwa kwa asilimia 81.29 ,makaravati ya kupitisha maji asilimia 96.3 na madaraja makubwa matatu kwa asilimia 100.
Mambo alieleza ,Tabaka la zege limefikia asilimia 40 ambapo jumla ya mradi umefikia asilimia 54.1 na utakamilika baada ya miezi miwili na nusu.
Alisema kulikuwa na changamoto ndogondogo lakini Serikali na TPA wameshamaliza ,na mkandarasi kishalipwa asilimia 33 na mradi ni wa Bilioni 36.
Kwa upande wake Alexander Ndibalema kutoka TPA ,alieleza kati ya heka 502 ,wameshazungusha uzio heka 60 una urefu wa km.2.96 ,heka 5 wameziendeleza kwa Ajili ya Bandari na kazi imefanywa na SumaJkt .
Ndibalema alisema ujenzi unaenda Sambamba na ujenzi wa barabara kwa Ajili ya uingizaji mizigo, mizigo itakayofika bandari ya Kwala itakuwa inakwenda kwa njia ya reli ,na ujenzi umefikia asilimia 65 na utakamilika kwa miezi miwili na nusu.