Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Furahika Education Dkt. David Msuya akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
…………..
Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na mafunzo ya kozi Uuguzi (Nursing) ngazi ya cheti yanayotolewa bure bila gharama yoyote na Chuo Furahika Education Tanzania kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam kupitia mradi wa Msaidie Mama Mjamzito.
Ili kuhakikisha vijana wengi wananufaika fursa hiyo uongozi wa Chuo cha Furahika Education wameongeza muda wa siku saba wa kutuma maombi ya kujiunga na chuo kuanzia tarehe 20.5.2022 hadi tarehe 28.5.2022.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Furahika Education Dkt. David Msuya, amesema kuwa wameongeza muda ili kuwapa fursa vijana waweze kupata elimu ya kozi uuguzi.
“Sifa ya wanafunzi ili ajiunge na kozi ya uuguzi lazima awe amepata Biology kuazia alama D , na mafunzo yanatarajia kuanza mwezi huu tano mwaka 2022” amesema Dkt. Msuya.
Ameeleza kuwa mradi wa Msaidie Mama Mjamzito utachukua wanafunzi zaidi ya 100 baada ya kumaliza masomo ya uuguzi kwa muda wa mwaka mmoja watakwenda kufanya kazi katika vijini mbalimbali watakavyopangiwa.
“Baadhi ya wahitimu baada ya mafunzo watapelekwa vijijini kwenda kuhudumia wagonjwa mbalimbali ambao wana hudumiwa na shirika’’ amesema.
Amefafanua kuwa wazazi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kuwapa elimu vijana wao, kwani itawasaidia katika maisha na kupiga hatau katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Chuo cha Furahika Education kimesajili na VETA na wanatoa kozi mbalimbali bure bila kulipa ada, hivyo wananfunzi wanachangia ada ya mitihani wanayofanya ili waweze kupata cheti.
Lengo la Chuo ni kuwaendeleza kielimu watoto wa kike na vijana kuwapa ujuzi mbalimbali kwa ajili ya mafanikio yao na familia kwa ujumla, fomu za kujiunga na chuo zinapatikana online kupitia website ya chuo.