Na Mwandishi wetu, Dar
Mkutano wa 19 Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kutoka katika Bara la Afrika na Nordic unatarajiwa kufanyika Helsinki, Finland kuanzia tarehe 13 – 15 Juni, 2022. Mkutano huo utakutanisha Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kutoka katika bara la Afrika na nchi za Finland, Norway Denmark, Iceland.
Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan amebainisha hayo alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mhe. Swan amesema mkutano huo utajadili masula ya amani na usalama, maendeleo endelevu na ushirikiano kati ya nchi za NORDIC na Afrika.
“Mkutano huo utajadili masuala ya amani na usalama, kuhusu umuhimu wa umini pamoja maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi,” amesema Balozi Swan.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema mkutano huo
umekuwa ukifanyika kila mwaka lakini kutokana na Janga la ugonjwa wa Uviko 19, mkutano huo haujafanyika tangu ulipofanyika mara ya mwisho nchini mwaka 2019.
Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Dkt. Donald Wright.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani katika sekta za Afya, Elimu, biashara na uwekezaji.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiurikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi. Talha Waziri wakifuatilia kikao cha Mhe. Waziri Mulamula na Balozi wa Finland
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini, Dkt. Donald Wright
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani hapa nchini, Dkt. Donald Wright. Kulia mwa Balozi Mulamula ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiurikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi. Talha Waziri na Afisa kutoka Wizarani Bibi. Kisa Mwaseba.