Naibu Katibu Mkuu mpya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi, akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo (hawapo pichani) alipokuwa anakaribishwa katika Wizara hiyo, leo Mei 23, 2022, jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu mpya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi, akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo alipokuwa anakaribishwa katika Wizara hiyo, leo Mei 23, 2022, jijini Dodoma. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo katika hafla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya katika Wizara hiyo, leo Mei 23, 2022, jijini Dodoma. Kulia meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu huyo, Dkt. Maduhu Kazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (katikati), Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Dkt. Maduhu Kazi (kushoto), na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Emmanuel Kayuni (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, baada ya kukabidhi ofisi kwa Dkt. Kazi, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
************************8
Na Mwandishi Wetu, MOHA, Dodoma.
NAIBU KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi amewashukuru Wakuu wa Idara na Vitengo kwa kumkaribisha katika Wizara hiyo, na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi.
Dkt. Kazi ambaye hivi karibuni aliteuliwa katika nafasi hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan na kuapishwa Mei 21, 2022 Ikulu jijini Dodoma, amekaribishwa na Viongozi hao na kuelezea majukumu yao wanayoyafanya Wizarani hapo, katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, Mtumba, jijini humo, leo Jumatatu Mei 23, 2022.
“Nimefurahi sana kuzungumza nanyi leo pamoja na kunikaribisha, naomba tufanye kazi kwa ushirikiano na pia tuwe wabunifu katika utendaji wetu wa kazi,” alisema Dkt. Kazi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio akizungumza kuhusu uteuzi wa Naibu katibu Mkuu huyo, amefurrahi kwa kiongozi huyo kuteuliwa katika Wizara hiyo, na kuwataka Wakuu wa Idara kumpa ushirikiano katika majukumu yake ya kazi ndani ya Wizara hiyo.
“Tumemfahamu na tumemsikia Naibu Katibu amezungumza nanyi, Wakuu wa Idara na Vitengo mmeeleza majukumu yenu na amewasikia, ataendelea kuwajua zaidi, tuendelee kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake,” alisema Kadio.
Wakuu wa Idara na Vitengo walijitambulisha, pamoja na kuelezea majukumu yao na changamoyo zinazowakabili na pia kumwelezea Naibu Katibu Mkuu huyo, kutokana na ongezeko la Bajeti ya Wizara katika Mwaka wa Fedha ujao wanatarajia sehemu kubwa ya changamoto zao zitatatulia.
Aidha, Dkt. Kazi amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, ambaye amehamishiwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI.