Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha na baadhi ya viongozi kutoka nchi mbalimbali walioshirikia Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa Majiji uliomalizika Mei 22, 2022 katika mji wa Kisumu nchini Kenya.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Katibu Mkuu wa Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa) Jean Pierre Elong Mbassi (Kulia) wakati wa mkutano wa tisa wa kimataifa wa Majiji uliomalizika katika mji wa Kisumu nchini Kenya Mei 22, 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Mawaziri wa Eswatini wakati wa Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa Majiji uuliomalizika katika mji wa Kisumu nchini Kenya Mei 22, 2022
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa ameshikilia Tuzo ya Heshima iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa) kwa Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa tisa wa kimataifa wa Majiji uliofanyika Kisumu nchini Kenya.
*****************************
Kisumu, KENYA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshiriki mkutano wa tisa wa viongozi wa majiji huko Kusumu nchini Kenya.
Mkutano huo uliomalizika Mei 222, 2022 uliwakutanisha maelfu ya wadau ulijadili maendeleo ya miji Barani Afrika na ulifunguliwa kwenye mji wa Kisumu, Magharibi mwa Kenya.
Mbali na maelfu ya Wadau, Watalaam na Viongozi wa Miji waliokutana kwenye mkutano huo, viongozi kadhaa wa mataifa ya Afrika, pamoja na wale waliostaafu nao walihudhuria mkutano huo.
Aidha, kupitia mkutano huo Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula alikabidhiwa Tuzo ya Heshima (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government) kwa niaba ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa).
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo wa kimataifa maarufu kwa jina la Africities ni kuhusu hali ya miundo mbinu kwenye miji mbalimbali na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa miji hiyo.
Mameya wa miji mbalimbali, Mawaziri wa serikali za mitaa walihudhuria mkutano huo na kutafuta suluhu ya changamoto zinazowasumbua wakazi wa miji yao kama vile mipangilio mibaya ya majengo, mitaa pamoja na changamoto za upatikanaji wa umeme.
Huo ni mkutano wa kwanza kufanyika katika jiji ambalo lina wakazi kati ya Elfu 50 na Laki tano ambapo kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2009 lina watu 409,000.
Kauli mbiu ya mkutano huu ni mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063.
Majiji mengine ambao yamewahi kuandaa mkutano huu unaofanyika kila baada ya miaka mitatu tangu1998 jijini Abidjan, umewahi pia kufanyika jijini Johannersburg, Dakar Kule Senegal na Marakesh Nchini Morocco.