Prof. Maurice Mbago (mwenye bahasha) ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEA akifurahia jambo na Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe walipokutana katika ziara ya kukagua mradi shule Msingi Kisasa
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akimuongoza Prof. Maurice Mbago Mwenyekiti wa Bodi ya TEA na ujumbe wake katika ukaguzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa shule ya msingi Kisasa.Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye, akimuongoza Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Prof. Maurice katika ziara ya kukagua mradi wa ukarabati na upanuzi wa shule ya Msingi Medeli Jijini DodomaMwalimu Mkuu w Shule ya Msingi Medeli, Bi Grace Lisasi akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TEA prof. Maurice Mbago alipofanya ziara katika shule hiyo kukagua maendeleo ya mradiMwenyekiti wa Bodi ya TEA Prof. Maurice Mbago, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye wakikagua ukarabati na upanuzi wa shule ya Msingi Medeli.
************
Mamalaka ya Elimu Tanzania (TEA) Imeendelea kuboresha miundombinu ya Elimu Jijini Dodoma kwa kuwezesha ukarabati na upanuzi wa shule nne za msingi.
Katika ufuatiliaji wa miradi mbalimbali inatotekelezwa na TEA, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA), Prof. Maurice Mbago ametembelea mradi wa utanuzi na ukarabati wa shule nne za Msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofadhiliwa na TEA na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo uliogharimu Sh. Bilioni 1.9
Katika ziara hiyo ya siku moja Prof. Mbago, ametembelea shule ya msingi Medeli na Kisasa ambazo ni miongoni mwa shule nne zilizofadhiliwa na TEA.
Shule nyingine zilizifadhiliwa ni Mlimwa C na Kizota.
Waalimu wakuu wa shule za Msingi Medeli Bi. Grace Lisasi na shule ya Msingi Kisasa Bi. Jesca Mwarabu wamesema mradi huo umesaidia kuongeza ufaulu na udahili wa wanafunzi.
Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amepongeza TEA kwa ufadhili huo ambao amesema umeboresha mwonekano miundombinu na mandhari za shule nufaika.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye amehimiza wanufaika wa mradi huo kutunza vizuri miundombinu hiyo kwa manufaa ya watanzania.