Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Ilala, Lilian Mwombeki Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya siku ya vipimo duniani ambayo huadhimishwa Kila tarehe 20 Mei ya Kila mwaka, Ofisi kwake Ilala Boma Jijini Dar es salaam
Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Ilala, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya siku ya vipimo duniani ambayo huadhimishwa Kila tarehe 20 Mei ya Kila mwaka
Timu ya wakala wa vipimo Mkoa wa Ilala ikiongozwa na meneja Lilian Mwombeki wakifanya ukaguzi wa kuangalia usahihi wa vipimo katika kampuni ya FM J Hardware LTD, iliyopo Buguruni Jijini Dar es salaam, leo Ijumaa Mei 20, 2022
Afisa Mauzo kutoka FM J Hardware LTD, Athman Kanyerere akimtembeza Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala Lilian Mwombeki , maeneo mbalimbali baada ya kuwasili katika kampuni hiyo kwaajili ya ukaguzi wa usahihi wa vipimo , leo Ijumaa Mei 20, 2023
Afisa vipimo mkoa wa kivipimo Ilala, Denis Mtatiro akihakiki usahihi wa vipimo katika bidhaa za kampuni ya FM J Hardware LTD ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya vipimo Duniani ambayo huadhimishwa Mei 20 kila mwaka
*********************
Katika kuadhimisha siku ya vipimo duniani yenye kauli mbiu inayosema ‘Matumizi ya Vipimo Kidigitali’, Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala imetoa wito kwa wafanyabiashara kutumia vipimo vilivyo sahihi kwa njia ya kidigitali ili kuweza kurahisisha biashara zao na kuongeza thamani ya pesa kwenye shughuli zao za kilasiku.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa Kila tarehe 20 Mei ya Kila mwaka, Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Ilala, Lilian Mwombeki amesema wao Kama Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala wanatumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwa wafanyabiashara mbalimbali ili kuweza kutumia vipimo sahihi wakati wa biashara zao;
“Sisi kama Wakala wa Vipimo tunaadhimisha kwenye maeneo tofautitofauti tunayofanyia kazi kwa kuwafundisha na wafanyabiashara jinsi ya kutumia vipimo sahihi sehemu mbalimbali”
Aidha Meneja huyo amesema kwa Mkoa wa Ilala wana sekta mbalimbali wanazifanya nao kazi hivyo kwa mwaka huu wameamua kuadhimisha siku ya Vipimo Duniani katika sekta ya biashara ya ujenzi;
“Kwa Mkoa wa Ilala tumeamua kuadhimisha kwenye maeneo tofauti yenye vifaa vya ujenzi kwasababu sisi Wakala wa Vipimo tuna sekta mbalimbali ambazo ni sekta ya Afya, Ujenzi, Kilimo, Biashara n.k hivyo kwa mwaka huu tumeamua kuchagua sekta ya Biashara kwenye upande wa ujenzi”
Kwa upande wake Afisa vipimo mkoa wa kivipimo Ilala, Denis Mtatiro amesema kwa Ofisi ya vipimo wanakuwa na ukaguzi wa mwaka, ukaguzi wa muda wowote, na ukaguzi wa kushtukiza ili kuhakikisha kwamba wanamlinda mlaji
Pia ameongeza kuwa Elimu wanayowapa wafanyabiashara ni namna bora ya ufungashaji ambao upo kwa mujibu wa Sheria ili kuweza kuwa na biashara shindani.
Naye Afisa Mauzo kutoka FM J Hardware LTD, Athman Kanyerere wanahitaji kumlinda mteja ambapo anapokwenda kununua bidhaa anakutana na ubora ambao anautarajia kwa kuhakikisha bidhaa inayokuja inafanana na size ambayo kiwandani imewapa
Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitahidi bidhaa wanayochukua kiwandani ifanane na uhalisia wa kile kipimo chenyewe ili kuepusha changamoto ndogondogo zinazojitokeza kwasababu mlaji wa mwisho anatakiwa atumie pesa yake kuendana na bidhaa yenyewe ilivyo.