Baadhi ya waigizaji wakitoa burudani katika kampeni ya uelimishaji jamii kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi katika kata 11 za Wilaya ya Bagamoyo Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye akizungumza katika kampeni ya uelimishaji jamii kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi katika kata 11 za Wilaya ya Bagamoyo Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Wilaya ya Bagamoyo Bi. Magreth Joseph akizungumza katika kampeni ya uelimishaji jamii kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi katika kata 11 za Wilaya ya Bagamoyo Baadhi ya wanafunzi wa shule za Sekondari wakifuatilia maigizo ya uelimishaji kuhsu masuala ya afya ya Uzazi yanayoendelea kutolewa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kushirikiana na Taasisi ya Bagamoyo Friendship Society ya Ujerumani katika kata 11 za Wilaya ya Bagamoyo.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
******************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kushirikiana na Taasisi ya Bagamoyo Friendship Society ya Ujerumani imetumia Sanaa ya maigizo kutoa elimu ya afya ya uzazi hasa madhara ya mimba za utotoni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kampeni hiyo ya uelimishaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye amesema kampeni hiyo imepanga kufikia takribani kata 11 zilizopo wilayani Bagamoyo na baadae kuhakikisha inawafikia jamii nzima kwa ujumla.
Amesema muitikio wa utoaji wa elimu hiyo umekuwa mkubwa kwani kumekuwa na ushirikishwaji wa jamii kwa kuuliza maswali pamoja na kutoa maoni yao kuhusu masuala ya afya ya uzazi hususan madhara ya mimba za utotoni.
“Kupitia Sanaa shirikishi itasaidia kutatua changamoto za mimba za utotoni zinazokidhiri katika jamii zetu zinazotuzunguka pia wengi watapata elimu ya afya ya uzazi kwa undani zaidi kwasababu tumekuwa tukishirikiana na wataalamu wa afya ya uzazi kwenye kampeni hii”. Amesema Dkt.Makoye.
Aidha Dkt.Makoye amesema kutokana na Serikali kutoa maelekezo kwamba vijana wa kike ambao bahati mbaya walipata ujauzito waweze kurudi shuleni, sasa wameona kuna umuhimu jamii ielimishwe kuhusu suala hili kwa maana baadhi ya watu katika jamii wamekuwa na imani potofu kwenye suala hili.
“Tumeona tuchukue hatua kueleimisha jamii kwamba hili suala ni lakawaida kwahiyo waweze kuwasaidia hawa vijana ambao kwa bahati mbaya walipata ujauzito basi waweze kurudi shuleni na wapewe msaada unaotakiwa kuanzia kwenye familia zao, kwenye jamii kwa ujumla pamoja na kwenye shule wanazokwenda kusoma”. Amesema
Naye Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Wilaya ya Bagamoyo Bi. Magreth Joseph amewataka wananchi kuunga mkono tamko la Mhe. Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwa wasichana waliokua shule mara watakapojifungua warudi shule kumalizia masomo yao kwa kuwa kila mmoja ana ndoto hivyo tuwasaidie wafikie ndoto zao.
“Vile vile vituo vya huduma za afya vina huduma wezeshi ambazo zitamfanya mtoto wa kike aweze kuhimili hali hio bila shida yoyote,” alisema Bi. Magreth.