Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wanafunzi na wadau mbalimbali waliofika chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha CDTI wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia.
Mkuu wa chuo cha CDTI Godfrey Mafungu akiongea na wanafunzi na wadau mbalimbali waliofika chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha CDTI wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia.
Na Fredy
Mgunda,Iringa.
Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amezindua kitengo cha dawati la jinsia
katika chuo cha maendeleo ya Jamii Ruaha CDTI kilichoanzishwa rasmi ili
kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi chuoni hapo
Akizunguma
wakati wa uzinduzi kitengo hicho, mkuu wa wilaya ya Iringa alisema kuwa uwepo
wa dawati hilo utachangia maendeleo ya usawa wa kijinsia na kupunguza vitendo
vya ukatili ikiwemo rushwa ya ngono inayotajwa kukithiri katika vyuo mbalimbali
na kuchafua taswira ya elimu ya kati na ya juu nchini.
Moyo
alisema kuwa uwepo wa kitengo hicho cha dawati la jinsia katika chuo hicho
kutachochoe usawa wa haki kwa wanafunzi wa chuo hicho cha Ruaha.
Alisema kuwa
Iringa kumeibuka wimbi kubwa kwa wanaume kuanza kufanyiwa vitendo vya ukatili
wa kijinsia na wanaume wameanza kutoa malalamiko yao kwenye vyombo husika hivyo
wanafunzi wa kiume kutoona aibu kulitumia dawati hilo pindi wanapotendewa
ukatili
“kitengo
hicho siyo kwa ajili ya wanafunzi wa kike pekee, huku akiwahimiza wanafunzi wa
kiume kutoona aibu kulitumia dawati hilo pindi wanapotendewa ukatili” alisema
Moyo.
Kiongozi
huyo amepongeza hatua ya uanzishwaji wa dawati hilo Chuoni hapo na kutoa mwito
kwa taasisi mbalimbali kuunga mkono jitihada zilizoanzishwa katika kupambana na
ukatili wa kijinsia chuoni hapo.
Moyo alizitaka
mamlaka nyingine kama vile jeshi la Polisi,TAKUKURU,ofisi ya mashtaka na
taasisi zisiszo za kiserikalina za serikali kuendelea kuunga mkono juhudi
zilizofanywa na chuo hicho kwa kutoa ushirikiano unatakiwa.
Kwa upande
wake mratibu wa dawati la jinsia katika chuo hicho cha maendeleo ya jamii CDTI
Asha Nyoni alisema kuwa Unzishwaji wa dawati hilo la jinsia umetokana na uwepo
wa taarifa za matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Taasisi za
Elimu ya juu na ya kati.
Nyoni alisema
kuwa maswala ya ukatili wa kijinsia ni mtambuka hivyo ni kuangalia kwa namna
gani ya kuweka mfumo rafiki ya kuona namna gani wanakomesha au kuondoa kabisa
vitendo vya ukatilii wa kijinsia.
Alisema kuwa
ukatilii wa kijinsia umekuwa ukitokeza maeneo mengi ya elimu ya juu na kati
ndio maana wizara ikaamua kuanzisha dawati la ukatilii wa kijinsia.
Awali mkuu wa chuo cha CDTI Godfrey Mafungu
ameeleza jitihada zilizoanzishwa na chuo hicho katika kuwawezesha wanafunzi
kujitambua na kuepukana na vitendo hatarishi
Mafungu alisema
kuwa umefika wakati kwa wanafunzi kujitambua kuhusu maswala ya ukatili wa
kijinsia kwa ajili ya maendeleo ya elimu wanayoipata chuoni hapo.
Alisema kuwa
imekuwa vigumu mno kwa vijana wengi kujitambua wawapo chuoni hivyo jambo la
kujitambua linatakiwa kupigiwa kelele sana ili vijana waweze kujitambua.
Mafungu alisema
kuwa ukatili wa kijinsia umekuwa unarudisha nyuma juhudi za kuleta maendeleo
kwa wananchi hivyo wanafunzi wa chuo wakiwa na elimu ya ukatilii wa kijinsia
basi wataifikisha kwa jamii husika juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia.
Hatua hii
ni utekelezwaji wa maelekezo ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati
akilihutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano ambapo alielekeza Taasisi za
Umma na Binafsi kuhakikisha zinaweka utaratibu unaofaa wa kutokomeza Ukatili
kwa wanawake, wasichana wavulana na watoto.