Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju akifunga Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara uliofanyika leo Mei 19,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Lameck Sendo akielezea namna Baraza hilo lilivyoshiriki kutoa maoni kwenye mapito ya Sera ya Wazee wakati wa Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara uliofanyika jijini Dodoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Nandera Mhando akielezea jambo wakati wa Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara uliofanyika jijini Dodoma.
Katibu wa Baraza la Ushauri la Wazee Taifa Bw.Anderson Lyimo,akizungumza wakati wa Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara uliofanyika leo Mei 19,2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara wakati wa Mkutano uliowakutanisha Viongozi hao kutoka mikoa ya Tanzania Bara uliofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara,Mohamed Bakari,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufungwa kwa Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara uliofanyika leo Mei 19,2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka mikoa ya Tanzania Bara mara baada ya kufunga Mkutano uliowakutanisha Viongozi hao jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
………………………………………….
Na WMJJWM- Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju amewaasa Wazee nchini kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatunza Afya zao kwa kujiepusha na mtindo ya maisha hatarishi.
Mpanju ameyasema hayo Mei 19, 2022 jijini Dodoma wakati akifunga Mkutano wa viongozi wa mabaraza ya Wazee kutoka Mikoa ya Tanzania Bara.
Alisema kuwa Wazee wanapaswa kuhakikisha wanajitunza kiafya ili waweze kutumika na Taifa kwani Wazee ni hazina kwenye masuala mbalimbali husuani kushauri tunapojenga uchumi wa nchi.
“Niwaombe wazee wangu tujitunze hasa katika Afya zenu, Afya ni muhimu sana kwani bado tunahitaji nasaha na mawazo yenu katika Sekta mbalimbali ili tuweze kufikia Maendeleo tuliyojiwekea kama Taifa” alisema Mpanju
Aidha Mpanju amemuagiza Kamishna wa Ustawi wa Jamii kuhakikisha Sera ya Wazee inayoboreshwa inapokea maoni na kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu na ili kuanza kwa mchakato wa utungwaji wa Sheria ya Wazee.
“Kuna mengine mengi mmeyasema ila mengi ya hayo yanahitaji Mwongozo wa Sera ya Wazee hivyo Sera hii ikikamilika hayo mengine yatafanyika na kutekelezeka kwa ufanisi” alisema Mpanju
Ameongeza kuwa Serikali itahakikisha wazee wanalindwa kwa kuhakikisha inaweka mifuno itakayosaidia kuwalinda na vitendo vya ukatili pamoja na kuwapa huduma Bora za Afya. Amewaasa pia familia, ndugu na jamaa kuwajibika kuwatunza Wazee wao ili wawe katika mazingira mazuri kwa Ustawi wao.
“Vijana tuwalinde na kuwatunza wazee wetu timizeni wajibu wenu kwani wakati wa ujana wao waliwatunza na kuwalea kama Watoto wenu” alisema Mpanju
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Amina Faki alisema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itahakikisha Wazee wanapata huduma kwa kuzingatia sheria na Sera zilizopo ili kutoa huduma chanya kwa Wazee ikiwemo huduma za afya, kushirikishwa na kuwakinga Wazee na vitendo vya ukatili.
“Katika kutoa huduma Bora za Afya Serikali imetenga jumla ya madirisha 5888 katika Vituo vya kutoa huduma za afya kote nchini zikiwemo Zahanati, Vituo vya Afya Hospitali za Wilaya Mkoa na Rufaa” alisema Bi. Amina
Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Lameck Sendo alisema Mkutano huo umetoka na maazimio ambayo yakitekelezwa kwa ufanisi na weledi Wazee nchini watapata ulinzi na huduma muhimu kwa Ustawi wao.
Akiyataja maazimio hayo ni pamoja na kuimarisha Baraza la Wazee Taifa, Wazee kulindwa na vitendo vya ukatili, Wazee kushirikiswa katika masuala mbalimbali katika jamii, kufutwa kwa Kodi mbalimbali kwa wazee na upatikanaji wa Huduma bora za Afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Help Age Daniel Smart alisema Shirika lake linaendelea kushirikiana na Serikali katika ngazi mbalimbali kuhakikisha inawezesha mabaraza ya Wazee kuundwa na kuweze kujiendesha kwa sababu umuhimu wa mabaraza hayo ni kuhakikisha Wazee wanakuwa na mfumo ambao utawasaidia kulindwa na kupata huduma muhimu.
Nao baadhi ya Wazee kutoka Mikoa ya Tanzania Bara wametoa Maazimio wakati wa Mkutano huo ikiwemo Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuendesha mabaraza ya Wazee, kuwajumuisha wazee katika masuala ya jamii, kupatikana kwa huduma ya Afya kwa Wazee wote na Wazee kupatiwa Pensheni ili ziweze kuendesha kupunguza changamoto za maisha.