Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhuhi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbi Gunze (kulia) akizungumza kwenye semina ya waandishi wa habari za mtandao (hawamo pichani) inayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar es salaam. (kushoto) ni Mkuu wa kitengo cha Leseni na mawasiliano (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka
Mkuu wa kitengo cha Leseni za Mawasiliano (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akitoa mada kwenye semina ya waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari za mtandao inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Maudhui (TCRA) Dereck Mrusuri akifafanua jambo alipokuwa akitoa mada kwenye semina hiyo inayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
**********************
*Yataka kuwa wabunufu wa vipindi
Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya MawasilianoTanzania (TCRA) imesema kuwa vyombo vya habari mtandaoni vinatakiwa kujenga uimara wake katika kutangaza maudhui ya kuenga jamii kuandaa vipindi vilivyo bora.
Akizungumza katika Semina ya Mafunzo ya Vyombo vya Habari vya Mtandaoni Mwenyikekiti wa Kamati hiyo Habbi Gunze amesema kuwa maudhui lazima yazingatiwe kwa weledi na sheria kwani vyombo hivyo kwa ajili ya jamii.
Amesema Teknolojia inakwenda kwa kasi hivyo vyombo vya habari mtandao vifanye kazi kuelimisha jamii na kuacha kuwa sehemu ya kupotosha ambapo sheria itatumika kudhibiti hali hiyo.
“Tutakwenda pamoja katika kutoa elimu katika kuhakikisha mnasimama na matokeo yake jamii itaelimika huku maendeleo yakionekana kutokana na kupata habari zinajenga zaidi” amesema Gunze.
Mjumbe wa Kamati ya Maudhui wa TCRA Dereck Mrusuri amesema kuwa vyombo vya habari mtandao vinatakiwa kubadilisha mtazamo wa kufanya kazi hiyo kwa kuwa na vipindi vinavyojenga na hatimae kuwa na uwezo wa kifedha na kujiendesha.
Amesema kuwa kuna watu wamefanikiwa vizuri katika kutengeneza vipindi vinavyojenga na jamii ikafuata na kupata mabadiliko ya kiuchumi kutokana na chombo cha habari kujikita katika kutatua changamoto ndani ya jamii.
Mrusuri amesema kuwa katika kufanya hivyo ni kuongeza ubunifu ambao watu wengine hawafanyi hivyo vyombo vya habari mtandaoni vina uwanja mpana zaidi katika eneo hilo.
Aidha amesema kuwa katika kufanya kazi kwa ustadi kwa vyombo vya habari kupitia waandishi kuzingatia masuala ya uvaaji kwani wakati mwingine mtu anaweza kudhalaulika kutokana na mavazi.
Mkuu wa Kitengo cha Leseni za Mawasiliank wa TCRA Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuna TV za mitandaoni kazi yake kuchukua vipindi vya nje ya nchi wakati leseni yake amechukua TCRA.
Amesema kuwa vipindi vingi watu wanatumia lugha ya kiingereza wanakwenda katika kutoa elimu kutumia lugha ya kiswahili kwani kiswahili kina maneno yakwenda kukidhi matamanio ya watazamaji.