Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe akizungumza wakati alipotembelea maabara ya vinasaba ya kufuatilia ugonjwa wa malaria mara baada ya kuizindua Leo kwenya makao makuu ya NIMR jijini Dar es salaam kulia ni Dr. Estee Torok kutoka taasisi ya BMGF ya Marekani na kushoto ni Rashid Mfaume Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe akikata utepe kuzindua maabara ya vinasaba ya kufuatilia ugonjwa wa malaria Leo kwenya makao makuu ya NIMR jijini Dar es salaam na Dr. Estee Torok kutoka taasisi ya BMGF ya Marekani na kushoto na Rashid Mfaume Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe akipata maelezo wakati alipotembelea maabara ya vinasaba ya kufuatilia ugonjwa wa malaria mara baada ya kuizindua Leo kwenya makao makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam katikati ni Rashid Mfaume Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
………………………………..
TAASISI ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Leo Mei 19, imezindua Maabara ya kisasa ya kufuatilia vinasaba vya ugonjwa wa malaria nchini, tukio lilifanywa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe aliyemwakilish Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Katika tukio hilo, Mganga Mkuu wa Serikali Dr.Aifello Sichalwe amesema kwamba maabara hiyo ni moja ya mkakati wa Wizara ya Afya kupitia mpango wa kudhibiti malaria kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Hata hivyo amesema kuwa Mradi huo wa maabara ya ufuatiliaji wa vinasaba vya malaria una lengo la kupata ushahidi wa kina juu ya chanzo kinachosababisha ugonjwa wa malaria nakwamba utasaidia wataalamu wa masuala ya tafiti kupata suluhisho namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.
“Utafiti huu wa vinasaba vya malaria ni wa awamu ya kwanza kutekelezwa hapa Nchini, na unafadhiliwa na wadau wetu wa maendeleo ikiwemo umoja wa Ulaya (UN),
tunawaomba waendelee kufadhili, pia tunaendelea kufanya mazungumzo na wadau wengine waweze kufadhili ile uwe endelevu nakufikia lengo tulilokusudia” amesema Dkt.Sichalwe.
Aidha, Dkt Sichalwe ameendelea kufafanua kwamba utafiti huo utasaidia kuwajengea uwezo NIMR Kwa kuzalisha takwimu za vinasaba vya Maleria hapa Nchini nakuzichakata kisha wizara ya afya itazitumia kufanya maamuzi ikiwemo kuandaa miongozo, kutunga sera nakutekeleza mikakati mbalimbali yakupambana na malaria huku wakiwa na ushahidi wa kisayansi.
Awali makamu mwenyekiti wa baraza la taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu ( NIMR) Dkt. Khadija Malima amesema kwamba utafiti wa vinasaba vya ugonjwa wa malaria utekelezaji wake umeanza tangu Mwezi Mei 2020 na inatarajiwa kukamilika mwezi oktoba 2023 ambapo kwa sasa umeanza katika mikoa kumi na tatu Nchini kote.
Amebainisha mkoa hiyo kuwa ni pamoja Dar es Salaam, Morogoro,Dodoma,Manyara,Pwani, Songwe, Ruvuma, Tabora, Tanga, Kagera, Mtwara, Kigoma, Mara.
Na kuongeza kwamba wasimamizi wakuu wa utafiti huo wa vinasaba vya malaria ni waganga wakuu wa mikoa pamoja Afisa afya.
Aidha maabara imeshakamilika na inaenda kufanya kazi iliyokusudiwa ili kusaidia kuleta suluhisho la ugonjwa huo ambao umekuwa ukipoteza idadi kubwa ya watu
Hata hivyo, Serikali imesema itahakikisha inaongeza jitihada za kutokomeza ugonjwa wa malaria ambao umekuwa tishio na kusababisha vifo vya watu wengi kila siku.