Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza Dr, Sebastiani Pima akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio uliofanyika leo kwenye Zahanati ya Mkolani.
Wazazi,walezi wakiwa na watoto wao waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio katika Wilaya ya Nyamagana
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (mwenye nguo ya kitenge) akimdondoshea mtoto matone mdomoni ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa chanjo ya polio katika Wilaya ya Nyamagana
……………………………………………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amezindua kamapeni ya chanjo ya polio katika Wilaya hiyo ambayo imeanza leo May 18 -21,2022.
Uzinduzi wa kampeni hiyo yenye kauli mbiu “Kila tone la chanjo ya polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza” umefanyika leo Ijumatano May 18,2022 kwenye Zahanati ya Mkolani iliyoko Wilayani humo Jijini Mwanza.
akizungumza kwenye uzinduzi huo Makilagi amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuongeza Kinga kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano ili kuweza kuzui maambukizi mapya ya ugonjwa wa polio.
Makilagi amesema kuwa baadhi ya wazazi,walezi wamekuwa wagumu kuwapeleka watoto wao kupata chanjo mbalimbali wakidai kuwa zinamadhara hali inayopekekea watoto kupata ulemavu au kupoteza maisha.
“Chanjo hizi hazijaanza kutolewa Leo na kumekuwa na tabia kila chanjo inapotokea inapata ukinzani, niwasihi sana wakina mama msipuuze chanjo hizi kwani ni muhimu sana katika makuzi,afya bora kwa watoto”,amesema Makilagi
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza Dr.Sebastian Pima amesema kuwa wamelenga kuchanja Watoto 92,698.
Ameeleza kuwa chanjo hiyo ni salama kabisa haina madhara yoyote hivyo wazazi wajitokeze kwenye vituo vya kudumu na vya muda mrefu vilivyopo katika maeneo mbalimbali ikiwamo sokoni,vituo vya mabasi,shuleni,kwenye nyumba za ibada ili watoto waweze kupatiwa chanjo.
“Chanjo hii imekuwa tofauti na chanjo nyingine ambazo zimekuwa zilitolewa kwenye vituo vya afya peke yake lakini hii ya polio tunaitoa nyumba kwa nyumba hivyo wazazi toeni ushirikiano wa kutosha pindi watoa huduma wanapowafikia kwenye makazi yenu”,amesema Pima
Spichiodha Mkongwa,ni miongoni mwa waliofika kuleta Watoto kwaajili ya kupatiwa chanjo amesema kuwa amefurahi sana mtoto wake kupata chanjo ambayo itamsaidia kukabiliana na milipuko mbalimbali ya magonjwa yanayojitokeza.
“Mimi napenda chanjo kwa sababu ninajua umuhimu wake kwa Mtoto hivyo wanawake tunaposikia matangazo ya chanjo tujitokeze kwa wingi ili watoto waweze kupatiwa Kinga”, amesema
Nae Mariam Sabi Mkazi, wa Kata ya Mkolani ameseam kuwa chanjo ni haki ya msingi kwa watoto,japo kunabaadhi ya watu wanaona kuwa ni mbaya ila anaamini ni ukosefu wa elimu hivyo Serikali iendelee kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa chanjo.