…………………………………………………..
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Katika kuelekea mkutano mkuu wa 27 wa wanahisa Taasisi ya fedha ya CRDB benki imefanikiwa kupunguza asilimia sita ya mikopo chechefu kutoka kwa wateja wake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha katika kuelekea mkutano mkuu wa 27 ya wanahisa wa Benki hiyo, Mkurugenzi mkuu Mtendaji wa CRDB,Abdulmajid Nseleka amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza mikopo chechefu kutoka asilimia 9 Hadi 3 kwa mwaka 2019 Hadi 2022.
“Nakupitia hilo tumefanikiwa kupunguza riba kwa kuangalia sekta muhimu inayoleta tija kubwa kwenye uchumi wa nchi ambayo ni kilimo,”amesema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi Nseleka amesema lengo ni kugusa watu wengi walio kwenye sekta nzima ya kilimo ambapo wakulima wengi watafaidika na huduma wanazotoa benki ya CRDB.
Amesema wakulima hao watanufaika kwa kununuliwa pembejeo au vitendea kazi mbalimbali na sekta ya pili kunufaika ni pamoja na wafanyakazi ambao wamepunguziwa riba kutoka asilimia 18 Hadi 13 huku wanawake wajasiriamali wapunguziwa kutoka asilimia 20 Hadi 12.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CRDB,Ally Laay amesema wamekuwa wakiwekeza elimu kwa wateja wao ikiwemo wanahisa ambo wapo zaidi ya laki sita.
“Kwa kuwekeza elimu kwa wateja itasaidia kuelewa umuhimu wa kuwekeza na namna ya kutumia fursa zinazojitokeza katika Benki ya CRDB lengo ni kumfikia Mwananchi mzawa nakutumia fursa zilizopo,”alisema Mwenyekiti huyo.
Naye Mkurugenzi wa mawasiliano, Tully ester Mwampamba aliwataka wanahisa kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura katika mtandao wao kuwachagua Wajumbe wa bodi ya wanahisa kuanzia Mei 18,2022.