Baadhi ya viongozi wa mashindano ya mbio za magari za Atlantic Mkwawa Rally of
Iringa wakiongea na waandishi wa habari juu ya ubora wa mashindano hayo mwaka huu
Baadhi ya viongozi wa mashindano ya mbio za magari za Atlantic Mkwawa Rally of
Iringa wakiongea na waandishi wa habari juu ya ubora wa mashindano hayo mwaka huu
Na Fredy
Mgunda,Iringa.
Mashindano ya mbio za
magari yanatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi na Jumapili Mkoani iringa katika
mashamba ya Mt Huwel Kwa kuhusisha jumla ya madereva 15 kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi
Wa habari Mkoani Iringa mwenyekiti wa IMSC Amjad Khan alisema mashindano hayo
yatafanyika Kwa Siku mbili kuanzia tarehe 21na 22 Mwezi wa tano mwaka huu 2022
siku ya Jumamosi na Jumapili.
Khan alisema kuwa
mashindano yamekuwa na msisimko mkubwa na mashabiki wengi wa Mkoa wa Iringa na
nje ya Mkoa wa Iringa hivyo Wananchi wanatakiwa kuwa makini ili kuepusha ajali
barabarani.
Alisema kuwa
wanejipanga kila eneo kuhakikisha usalama wa barabarani unakuwepo kwa Wananchi
na watazamaji wa mashindano hayo hivyo Wananchi wanatakiwa kujitokeza Kwa wingi
kushangilia.
Khan alisema kuwa
mashindano hayo mwaka huu yanajulikana kwa jina la Atlantic Mkwawa Rally of
Iringa.
Kwa upande wake Mtendaji
mkuu wa mashindano hayo Hidaya Kamanga alisema kuwa eneo ambalo mashindano
yatafanyika lina ukubwa wa kilometa 116 na kilometa 105 ndio ambazo zitatumika
katika ushindani wa magari siku Hiyo.
Kamanga alisema kuwa
wanawakaribisha Wananchi wote na wadau wa mashindano ya magari kwa kuwa usalama
umeimalishwa Kwa kiasi kikubwa na upo chini ya jeshi la polis mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa jeshi la
polisi litatoa elimu Kwa Wananchi juu ya usalama barabarani wakati wa
mashindano ya Atlantic Mkwawa Rally of Iringa Kwa lengo la kuepusha ajali
zisitokee Kwa Wananchi.
Kamanga alisema kuwa
Kwa upande usalama wa afya wamejipanga vizurii Kwa kuwa na madaktari wakati
wote wa mashindano hayo Kwa ajili ya kuwatibu majeruhi kama wakitokea.
Alisema kuwa
mashindano hayo ya mzunguko wa pili yatakuwa ya ushindani kweli kweli hivyo
Wananchi wajitokeze kupata furaha siku Hiyo.