Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) Erick Hamisi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa bandari kilichofanyika leo Jijini Tanga |
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) Erick Hamisi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa bandari kilichofanyika leo Jijini Tanga |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa kikao hicho |
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia akizungumza wakati wa kikao hicho |
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia akizungumza wakati wa kikao hicho |
Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho |
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Wakala wa meli nchini (TASAC) Kaimu Abdi Mkeyenge
akiuzungumza mara baada ya kumalizika kikao hicho
Sehemu ya Washiriki kwenye kikao hicho
Wadau wa kikao hicho
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
SERIKALI
ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imetoa sh.Bilioni
500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kuhudumia mizigo ili kuongeza
ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa leo na
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) Erick Hamisi
wakati wa mkutano wa wadau wa bandari unaofanyika Jijini Tanga ambapo
alisema uwekezaji huo unaokwenda kufanyika katika bandari hiyo ni mkubwa
ambao utafungua fursa kwa nchi na maziwa makuu kwa matumizi ya bandari
hiyo.
Alisema kuwa kuna mradi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwara
ambapo watapeleka mizigo ya nje katika nchi za Maziwa makuu (Transit)
baada ya serikali kuwekeza fedha hizo ambapo pia zitatumika kununulia
vifaa ili kuwezesha ufanisi huo.
“Tutakuwa na ujenzi wa bandari
ya nchi kavu ya kwara, isitoshe serikali ya awamu ya sita imewekeza
kiasi cha shilingi Bilioni 500 kwa mara moja uwekezaji ambao hauajwahi
kufanyika kwa mara moja hii inaonesha mhe Rais amedhamiria kuifanya
bandari yetu ifanye kazi kwa ufanisi,” alisema Hamissi.
Mkurugenzi
huyo alisema uwekezaji unaofanyika kwasasa katika miundombinu ya reli,
Bandari na kwenye maziwa inaoensha kwamba nchi zote zinazotuzunguka
hazitakuwa na chaguo lingine bali kutumia bandari ya Dar es salaam
karibu watu milioni 700 za nchi hizo.
Mkurugenzi huyo alisema
mkutano unaofanyika mjini Tanga kuwakutanisha wadau wa bandari haujawahi
kufanyika hivyo utatoa fursa kwa wadau kujadili vikwazo na fursa
zilizopo katika kuongeza ufanisi zaidi ya bandari zilizopo hapa nchini.
Awali
akiungumza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa meli nchini (TASAC)
Kaimu Abdi Mkeyenge alisema kwamba wadau wamekutanishwa pamoja ili
kutazama changamoto wanazokutana nazo kasha waweze kuzipatia majawabu ya
mapendekezo ya kuyafanyia kazi kwa pamoja.
Alisema warsha hiyo
itatazama changamoto mbalimbali ambazo zinaipata bandari ya Dare s
salaam na fursa zilizopo na kutoa mapendekezo ya kuboresha ikiwemo
bandari ya Tanga.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la
Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa, alisema mkutano huo wa wadau
utasaidia kuongeza fursa za usafirishaji mizigo utakaofanywa na shirika
hilo ambalo limefanya ukarabati wa reli yake ili kuweza kuhudumai nchi
za maziwa makuu.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wasafirishaji nchini
(TAT), Ashraf Khan alisema wao kama wasafirishaji wanaiomba bandari
iwasaidie maroli yao yanayobeba mizigo bandarini yaweze kutoka kwa
wepesi ili meli zinazoingia bandarini zichukue muda mfupi kukaa
bandarini.
Awali akifungua warsa hiyo ya siku mbili Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Adam Malima, aliwataka wajumbe wa mkutano huo ikiwemo uongozi
wa Bandari kutazama changamoto hizo na kuzipatia majawabu ili bandari ya
Dar es salaam iweze kushindana na bandari nyingine zilzopo katika
ukanda huu.
Alisema wanapofikiria kuondoa changamoto katika
bandari ya Dar es salaam wafuate maelekezo yanayotolewa na rais ili
waweze kuongeza tija lakini pia kushindana na bandari za Beira nchini
Msumbiji pamoja na ile ya Mombasa nchini Kenya.
“Kuweni mfano wa
kile ambacho Rais wetu anachohubiri kuitaka bandari ifanye kazi kwa
ufanisi, tusiwe watu wa kuiangusha bandari tufanye ifanye vizuri
kushindana na bandari nyingine,” alisema Mkuu wa mkoa huyo.