Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda wakikagua mabanda mbalimbali wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,akizungumza wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda ,akielezea umuhimu wa maonyesho hayo wakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga,akizungumza wakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Eliamani Sedoyeka,akizungumzawakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumzawakati wa maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,amevitaka vyuo vya elimu ya juu nchini kujiimarisha katika utafiti ili kupata maendeleo kwenye ugunduzi na ubunifu wa teknolojia zitakazosaidia Tanzania kupiga hatua zaidi.
Mhe.Othman ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Amesema kuwa vyuo vikuu kazi yao ya msingi ni utafiti na kutaka kujiimarisha kwenye eneo hilo na kuwa na sera bora za tafiti ambazo zitasaidia na kuchagiza wabunifu na wagunduzi kwa kulinda haki zao na kufaidi matunda ya kazi zao.
‘Natoa wito kwa Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar kuandaa mikakati maalum ya kulinda kazi mbalimbali za ubunifu”amesema Mhe.Othman
Mhe.Othman amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wiki hii na ndio maana maonesho haya yanafanyika ili kuendelea kuibua na kukuza vipaji tunapaswa kufanya maonesho naamini itatusaidia kuongeza kasi ya maendeleo kwa taifa.
Aidha amesema kuwa serikali zote mbili zimeazimia kujenga uwezo wa ndani wa kuendelea kuwekeza katika rasilimali watu, miundombinu na vifaa vya kisasa vya utafiti na ubunifu pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Taasisi za Sayansi na Teknolojia na sekta ya viwanda.
”Serikali zote mbili ya Muungano na Zanzibar zinatambua umuhimu na mchango wa ubunifu na teknolojia katika kurahisha na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za mbalimbali za kiuchumi na kijamii.”amesema Mhe.Othman
Ameongeza kuwa ubunifu ukitumika vyema ni nyenzo na kichecheo muhimu cha maendeleo ya haraka katika sekta za huduma, jamii na uzalishaji na ndio maana Serikali inaendeleza bunifu hizo.
“Serikali itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha na kitaalamu COSTECH, ili iweze kusaidia zaidi shughuli za utafiti na ubunifu nchini kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Mhe.Othman
Pia Makamu wa Rais amepata fursa ya kutembelea na kujionea bunifu mbalimbali zilizopo katika mashindano hayo na kuvutiwa na bunifu hizo.
Hata hivyo Mhe.Othman ameishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa Maonesho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa mwaka huu wa 2022 huku ikiwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa maendeleo endelevu”
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,amesema kuwa Taasisi tofauti tofauti 50 pamoja na wabunifu 26 ambao bunifu zao zimefikia hatua ya kuingia sokoni na kuanza kutumika zimeshiriki katika maeonesho hayo.
‘Amesema kuwa wabunifu 862 walijisajili kwa mwaka huu na wabunifu 86 bunifu zao zitashindanishwa ili kupata washindi.”amesema Prof.Mkenda