Na Farida Said.Morogoro.
Jamii imetakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ili kukabiliana na majenga ya moto yanayojiotokeza katika maeneo yao ya makazi na ofisi pamoja na kuacha kukimbili majanga yanapojitokeza.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Wakili Albert Msando aliposhiriki zoezi la utayari wa kukabiliana na majanga ya moto lililoandaliwa na benki ya NMB katika kituo chake cha kibiashara cha mjini Morogoro.
Wakili Msando alisema ni lazima wananchi wachukue tahadhari ikiwemo kuacha kujenga nyumba kiholela hali inayosababisha kushindikana kwa udhibiti wa moto pindi majanga yanapojitokeza.
Naye Meneja wa kituo hicho cha biashara za Benki hiyo Bwana Hamis Issa amesema tukio hilililoandaliwa na kituo chake ni la kuwaweka wafanyakazi wake pamoja na wananchi tayari kama njia ya kuwafahamisha kuwa majanga ya moto yanaweza kujitokeza wakati wowote huku akiwataka wananchi kuzikatia bima biashara zao pamoja na makazi.
Alizipongeza taasisi zote za serikali zilizojitokeza katika tukio hilo ili kuudhibiti moto huo pasipo kujua kuwa ni tukio la kutengenezwa lakini zilitimiza wajibu wao kwa weledi.
Akizungumzia tukio hilo mwakilishi wa mkuu wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro Mkaguzi Emmanuel Ochieng amesema amefurahishwa nalo kwakua limezidi kuwaweka tayari katika kukabiliana na majanga ya moto.
Aliongeza kuwa kazi ya jeshi lake inahitaji utayari wa mara kwa mara na wakati wote hivyo kwa tukio hilo limewaimairisha na kuwakumbusha kuwa majanga ya moto kamwe hayapigi hodi.