Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Ukaguzi kwa Kuzingatia Vihatarishi (Risk Based Audit) kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) yanalenga kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Ndani katika kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi taratibu mbalimbali za ukaguzi na kushauri kwa Maafisa Masuuli.
(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina).
Mkaguzi Mkuu wa Ndani, CPA Magdalene Kirumba akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Ukaguzi kwa Kuzingatia Vihatarishi (Risk Based Audit) kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) yanalenga kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Ndani katika kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi taratibu mbalimbali za ukaguzi na kushauri kwa Maafisa Masuuli.
(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)
Baadhi wa washiriki wa mafunzo ya Ukaguzi kwa Kuzingatia Vihatarishi (Risk Based Audit) kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika Taasisi, Wakala wa Serikali na Mashirika ya Umma, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya mgeni rasmi, Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani katika kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi taratibu mbalimbali za ukaguzi na kushauri kwa Maafisa Masuuli.
(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Ukaguzi kwa Kuzingatia Vihatarishi (Risk Based Audit) kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali, leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani katika kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi taratibu mbalimbali za ukaguzi na kushauri kwa Maafisa Masuuli.
(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mafunzo ya Ukaguzi kwa Kuzingatia Vihatarishi (Risk Based Audit) kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika Taasisi, Wakala wa Serikali na Mashirika ya Umma leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) yanalenga kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Ndani katika kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi taratibu mbalimbali za ukaguzi na kushauri kwa Maafisa Masuuli.
(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto ( wa pili kushoto) akifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Ukaguzi kwa Kuzingatia Vihatarisha kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), jijini Arusha leo. Kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Magdalene Kirumba. Wengine pichani ni Xavery Komba, Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Mfuko wa Self na Linus Kakwesigabo, Afisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina.
(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina).
**************************
Na Mwandishi Maalumu, Arusha
MSAJILI wa Hazina, Mgonya Benedicto amewataka watendaji wakuu wa taasisi, mashirika ya umma na wakala za Serikali kutekeleza kwa wakati mapendekezo yanayotolewa na Wakaguzi wa Ndani ili kudhibiti na kuondoa athari za vihatarishi katika taasisi wanazozisimamia.
Kauli hiyo imetolewa na Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto leo (Jumatatu) jijini Arusha kwenye ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi kwa kuzingatia vihatarishi (Risk Based Audit) kwa wakaguzi wa ndani 474 kutoka katika Taasisi, Wakala wa Serikali na Mashirika ya Umma 237 yaliyo chini ya Msajili wa Hazina.
Msajili alisema kwamba menejimenti ikisikiliza ushauri unaotolewa na wakaguzi wataweza kuimarisha na kudhibiti mifumo ya ndani na kuondoa mianya ya ukiukwaji wa Sheria,Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyowekwa na hivyo kuleta tija katika huduma na mrejesho wa uwekezaji unaotarajiwa serikalini.
“Kunapokuwa na udhibiti wa ndani madhubuti, Taasisi itafanya kazi zake kwa tija na kuwasilisha mapato yanayotarajiwa na kuwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali iliyopangwa kufanyika, na pia kutoa huduma bora kwa wananchi,” alisema Benedicto.
Pia amewataka Wakaguzi wa Ndani ambao amewaeleza kuwa ndio jicho katika taasisi na mashirika, kuyatilia maanani mafunzo hayo ili kwenda kuzisaidia taasisi wanazozikagua kwa kuwashauri juu ya kuimarisha udhibiti waifumo ya ndani.
“Ni imani yangu kwamba mafunzo haya yatawasaidia Wakaguzi wa Ndani wote watakaojengewa uwezo kwa kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi taratibu mbalimbali za ukaguzi na kuwashauri kwa makini Maafisa Masuuli ipasavyo,” alisema.
Alisema ofisi yake ambayo ina jukumu la kusimamia Uwekezaji wa Serikali na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya uendeshaji na uwekezaji katika Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala wa Serikali na Kampuni ambazo Serikali ni Mbia ilipanga mafunzo hayo kutokana na pendekezo la wakaguzi hao wakati wa mafunzo yaliyopita ya mfumo wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi yaani (GARI ITS) yaliyofanyika katika mwaka wa fedha wa 2020/21.
“Katika usimamizi wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala wa Serikali, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeona ni vema iendeshe mafunzo yanayohusiana na ukaguzi wa kuzingatia vihatarishi (Risk Based audit) kuwasaidia wakaguzi hao katika kuongeza uwezo wa utendaji kazi wao kiukaguzi na kuleta tija katika ushauri na mapendekezo wanayoyatoa kwenye Taasisi zenu,” alisema Msajili.
Aidha, Msajili aliwataka wakaguzi hao kuwaelimisha menejimenti juu ya kuzingatia vihatarishi na madhara yanayoweza kutokea iwapo vihatarishi havitazingatiwa na kudhibitiwa.
Msajili katika hotuba yake hiyo aliwapongeza wataalamu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina wakishirikiana na Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa mafunzo haya ambayo ni sehemu ya kuimarisha mifumo ya ndani ya udhibiti na usimamizi wa fedha za Umma katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali.
Aidha, aliwashukuru wadau wa maendeleo wanaofadhili Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) kwa kuwezesha kifedha kuhakikisha mafunzo hayo yanafanyika.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Ndani, CPA Magdalene Kirumba akimkaribisha Msajili wa Hazina kufungua mafunzo hayo alimshukuru kwa kutayarisha mafunzo hayo ambayo alisema ni muhimu kwa kuleta uelewa wa pamoja kuhusiana na dhana ya ukaguzi wa Ndani kwenye Mashirika ya Umma.
Alisema mafunzo hayo yataboresha ubora wa taarifa za ukaguzi na kupunguza hoja za ukaguzi kwenye sekta ya umma.
Alisema pamoja na kuwapa maarifa mapya, wakaguzi lengo jingine la mafunzo hayo ni kujenga uwezo kwa Wakaguzi wa Ndani kuhusu Miongozo ya Kimataifa (International Professional Practice Framework -IPPF) na namna ya kutumia miongozo hiyo katika kufanya kaguzi mbalimbali.
“Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatatatua changamoto za kutokuwa na matokeo yaliyotarajiwa katika kaguzi zinazofanyika (Audit approach) kwenye Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma,” alisema Kirumba.