Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akizungumza wakati akifungua kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia kwa niaba ya Waziri mkuu ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali (ICS) Kudely Sokoine,akitoa salam za ICS wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akizindua program Tumishi ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania iliyozinduliwa leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akiweka saini yake mara baada ya kuzindua program Tumishi ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania iliyozinduliwa leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akipata maelezo kuhusu programu hiyo kutoka kwa Meneja wa Programu hiyo ambaye pia ni Mtaalamu wa Malezi na Makuzi Bora ya Mtoto kutoka shirika la ICS, Sabrina Majikata mara baada ya kuzindua program Tumishi ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania iliyozinduliwa leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akiwa katika picha pamoja na wadau wa shirika la ICS mara baada ya kuzindua program Tumishi ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania iliyozinduliwa leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI pamoja lisilo la kiserikali la ICS wamezindua pragramu Tumishi ya Elimu ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania yenye lengo la kutoa elimu ya Malezi na Makuzi Bora ya mtoto kwa wazazi na walezi hao wenye watoto wa miaka 10 hadi 17.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma Mei 15, 2020 na Meneja wa Programu hiyo ambaye pia ni Mtaalamu wa Malezi na Makuzi Bora ya Mtoto kutoka shirika la ICS, Sabrina Majikata mara baada ya uzinduzi huo ulioenda sambamba na kongamano la Kitaifa la Malezi ya watoto na familia lenye kauli mbiu isemayo “Dumisha Amani na Upendo kwa Familia Imara: Jitokeze kuhesabiwa” amesema ParentApp inawalenga wazazi na walezi wenye watoto wa miaka kuanzia miaka 10 hadi 17.
Amesema kuwa katika siku hiyo wao kama shirika wameshirikiana na serikali kuweza kuzindua programu Tumishi kwa Malezi ya wazazi na walezi hapa nchini ambayo inatumia simu ya janja.
Bi.Sabrina amesema kuwa amesema kuwa mzazi au mlezi atapakua programu hiyo ambapo ataitumia bila kuwa na mtandao ambayo imetengenezwa mahususi wakati wowote wazazi na walezi hao watapata stadi za Malezi na Makuzi Bora ya mtoto.
Ameongeza kuwa serikali pamoja na wadau wamekuwa wakishirikiana kutoa elimu ya malezi kupitia makundi na kwamba changamoto ambazo wekutana nazo ni wazazi wengi kutokukutana kushiriki mafunzo wakiwa kwenye vikundi.
” Tumekuja na ubunifu huu kwa wazazi na walezi wakati wowote wakiwa huru kuweza kutumia program hii na kuweza kujifunza. Programu hii inaweza kuwapunguzia mzazi au mlezi kuondokana na changamoto anazozipata kama tunavyotambua changamoto za malezi mara nyinyi wamekuwa wakizidiwa na kushindwa kuzitatua,” amesema Sabrina.
Aidha amesema kuwa programu hiyo pia inaweza kumpa fursa mzazi kujifunza njia mbalimbali za kuondokana na msongo wa mawazo anayoyapata kwa sababu ya changamoto za malezi ya mtoto na kumpa dondoo za namna gani anaweza kumsaidia kijana wake.
Ametolea mfano serikali inavyohangaika na vijana wanaojiita Panya Road ka na kusema kuwa hilo ni tatizo ambalo wazazi wameshindwa kutatua ndio maana wameenda kujiingiza katika makundi ambayo hayana faida.
“Tunaamini kuwa programu hii wakiitumia watajua ni kwa namna gani wanaweza kutumia kwa vijana wao ili waweze kuwaokoa katika hatua waliyofikia,” amesema .
Hata hivyo amesema kuwa hatua wanayoipiti vijana hao ni hatua ya malezi na ukuaji ambayo inachangamoto nyinyi na inahitaji wazazi kuwa na stadi za kutosha ili kuwasaidia watoto hao kuweza kuvuka hatua hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima,amelipongeza Shirika hilo kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
”SIsi kama Serikali tunawapongeza ICS kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika
kutekeleza afua zinazohusiana na kuimarisha na kujenga uchumi katika ngazi ya kaya na jamii, stadi za malezi na makuzi bora ya mtoto kwa wazazi/walezi pamoja na kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto, kutokomeza ukatili wa kijinsia, kuboresha mazingira ya usalama wa watoto ndani na nje ya shule,”amesema Dk.Gwajima
Dk.Gwajima amesema kuwa anatambua kuwa ICS wanendelea na kutekeleza miradi mbalimbali katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Kilimanjaro.
Naye Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali (ICS) Kudely Sokoine,amesema kuwa shirika hilo limejikita katika kushirikiana na serikali kutekeleza afua zinazohusiana na kuimarisha na kujenga uchumi katika ngazi ya kaya na jamii, stadi za malezi na makuzi bora ya mtoto kwa wazazi/walezi na kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto.
Bw. Sokoine amesema,shirika hilo linaamini msingi wa Taifa lolote imara na lenye nguvu kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiroho unaanza katika familia.
“Katika kuadhimisha siku hii ya kimataifa ya familia Sisi kama ICS tunaamini ni katika familia ndiko watoto wanakofundishwa na kupandikizwa maadili mema, upendo, utu, heshima, uwajibikaji, uzalendo na kuipenda jamii na taifa lao kwa ujumla.”amesema Kudely na kuongeza kuwa
“ Na kwa msingi huo tunapokua na familia zilizo bora zinaunda jamii bora na jamii bora zinaunda taifa imara.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema,katika kuunga juhudi za kujenga familia bora na Taifa imara ,shirika hilo linashirikiana na Serikali katika kutekeleza mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Katika maeneo 8 (thematic areas) sisi tunatekeleza 6 na timu ya Wizara imeshafika Mkoani Shinyanga zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti wakaenda mpaka vijijini kabisa kukutana na wananchi na kuona jinsi tunavyotekeleza mpango huu kwa vitendo na matokeo yanayopatina. “ameeleza Bw.Sokoine