Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk.Dorothy Gwajima,akiwa na viongozi wa machinga wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan baada ya kupiga simu moja kwa moja na kuzungumza na wamachinga wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt. Zainabu Chaula,akizungumza wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira ,akizungumza wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.
……………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Wamachinga nchini kuwa katika mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai Ofisi yake kupitia Tawala za mikoa na Serikali za mitaa itatoa Sh. Milioni 10 kwa kila mkoa kuwezesha shughuli za machinga nchini.
Rais Samia amesema hayo leo Mei 16,2022 jijini Dodoma kwa njia ya simu mara baada ya kupiga simu moja kwa moja na kuzungumza na wamachinga waliohudhuria mkutano wa mafunzo ya viongozi wa Machinga nchini (SHIUMA).
Rais Samia amewahakikishia kuwapa ushirikiano Wamachinga nchini kwa kufanya kazi zao bila shida kwenye mazingira mazuri.
“Nakushukuru Waziri kwa kuwapa Wamachinga Ofisi ambayo ni jengo la Serikali,nimesikiliza hotuba yao na nimefurahishwa,nawahakikishia ushirikiano na mazingira mazuri na ifikapo mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai nitatoa milioni kumi kwa Kila mkoa kuwezesha shughuli zao,”amesema
Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dodoma kwa siku tano yakihusisha viongozi wa Machinga Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima,amempongeza Rais Samia kwa uamzi huo na kueleza kuwa umeleta tumaini jipya kwa Machinga nchini.
Hata hivyo amewataka Machinga kuhakikisha kuwa fedha hizo haziwi chanzo cha kuvuruga umoja wao badala yake wazitumie kwa kazi iliyokusudiwa na kuwepo uwazi utakaoonyesha zimetumika kwa matumizi gani.
Awali,Naibu Katibu Mkuu (SHIUMA) Joseph Mwanakijiji ameeleza kuwa kwa sasa wana mahusiano mazuri na serikali jambo ambalo linalosaidia Machinga anakuwa na mazingira mazuri na kuhakikisha anapangwa vizuri na kufanya biashara kwa uhuru.
Hata hivyo amesema wanachangamoto nyingi lakini kero ya miundombinu kwa baadhi ya masoko haiko sawa na kusababisha kiuchumi hawafikii malengo kwasababu baadhi ya miundombinu haiko sawa na kuhatarisha afya,ukosefu pia wa ofisi za Machinga na changamoto za kibajeti.
“Changamoto nyingine pamoja na stadi za biashara ,makazo bora,umilikishwaji wa maeneo ya machinga hivyo tunaomba kupewa barua ya idhini kuepuka kuondolewa mara kwa mara pindi halmashauri zinapo badili matumizi ya maeneo,amesema.
Mafunzo hayo ya Viongozi wa shirikisho la umoja wa Machinga Tanzania yameandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya jamii,Jinsia,wanawake na makundi maalumu kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo huku kaulimbiu yake ikiwa “Machinga ni fursa sahihi ya kukuza uchumi wa nchi yetu”.