Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akizungumza leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia kwa niaba ya Waziri mkuu ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,akizungumza wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt. Zainabu Chaula,akizungumza wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk. Fatma Mganga,akisalimia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali (ICS) Kudely Sokoine,akitoa salam za ICS wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akizindua program Tumishi ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania iliyozinduliwa leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akiweka saini yake mara baada ya kuzindua program Tumishi ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania iliyozinduliwa leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene,akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kufungua kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia kwa niaba ya Waziri Mkuu ambapo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
………………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu George Simachawene ameviagiza vyombo vyote vya sheria kuhakikisha mashauri yanayohusu kesi za watoto kufanyiwa kazi na kumalizika haraka ndani ya miezi sita.
Akizungumza leo Mei 15,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia kwa niaba ya Waziri mkuu.
Simbachawene amezionya familia ambazo zimekuwa na tabia ya kumaliza keshi zinazohusu watoto zenyewe bila kufikisha mashauri katika vyombo vya sheria kuacha mara moja.
“Waziri mkuu amenituma nitoe maagizo haya kwa vyombo vyote vya sheria nchini kuhakikisha kuwa mashauri yote yanayohusu watoto yanafanyiwa kazi na kutolewa maamuzi ndani ya miezi sita na siyo vinginevyo”amesema Simbachawene
Amesema kuwa hivi sasa matukio ya ukatili kwa watoto yamekuwa yakiongezeka na wahusika wakuu ni wanafamilia wenyewe.
“Pia wazazi wote ambao watabainika kumaliza wenywe kwa wenyewe mashauri yanayohusu ukatili dhidi ya watoto kama vile ubakaji,urawiti na mimba wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine”amesisitiza Simbachawene
Simbachawene amesema kuwa takwimu za ukatili mwaka 2021 kuanzia mwezi Januari hadi Desemba zinaonyesha jumla matukio 11,499 ya ukatili dhidi ya watoto na matukio makubwa yalioongoza ni ubakaji 5899, mimba 1977 na ulawiti 1114.
Hata hivyo amewataka watoto wote kutoogopa kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili iwe kwa walimu au kwa mtu yoyote.
‘’Msirubuniwe na kuendelea kuficha siri mtaharibikiwa na ndoto zenu zitapotea kama umefanyiwa ukatili toa taarifa kwa mtu utakayeona anaweza kukupa msaada wa haraka,’’amesisitiza Simbachawene.
Katika hatua nyingine Simbachawene amezindua program Tumishi ya ParentApp kwa wazazi/walezi wa Tanzania.
Program hiyo itawasaidia wazazi/walezi na watoto kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo katika jamii.
Ambapo utekelezaji wa majaribio ya awali na kushirikisha jamii,Serikali na watafiti umeshakwishaanza.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dk. Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali inatambua na inathamini familia kama chanzo cha nguvu kazi ya taifa.
Pia amesema kuwa wizara imeandaa muongozo wa malezi ya watoto kuanzia 0 hadi miaka 18.
“Hivyo katika kuimarisha uwezo wa familia katika kutimiza majukumu yake, serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali za kuwezesha familia kuishi kwa amani na upendo.”amesema Dk. Gwajima
Dk.Gwajima amesema kuwa baadhi ya afua hizo ni kutoa elimu ya malezi chanya kwa wataalam wa Halmashauri 7,445 wakiwemo Maafisa Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Maafisa Lishe na walimu.
Hata hivyo, amesema kuwa Tanzania inaungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila mwaka tarehe 15 Mei.
Ambapo Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika kimkoa ambapo mikoa yote 26 inafanya maadhimisho haya kwa utaratibu ambao wanaona unafaa kulingana na mazingira yao.
Awali Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali (ICS) Kudely Sokoine,amesema kuwa shirika hilo limejikita katika kushirikiana na serikali kutekeleza afua zinazohusiana na kuimarisha na kujenga uchumi katika ngazi ya kaya na jamii, stadi za malezi na makuzi bora ya mtoto kwa wazazi/walezi na kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto.
Bw. Sokoine amesema,shirika hilo linaamini msingi wa Taifa lolote imara na lenye nguvu kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiroho unaanza katika familia.
“Katika kuadhimisha siku hii ya kimataifa ya familia Sisi kama ICS tunaamini ni katika familia ndiko watoto wanakofundishwa na kupandikizwa maadili mema, upendo, utu, heshima, uwajibikaji, uzalendo na kuipenda jamii na taifa lao kwa ujumla.”amesema Kudely na kuongeza kuwa
“ Na kwa msingi huo tunapokua na familia zilizo bora zinaunda jamii bora na jamii bora zinaunda taifa imara.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema,katika kuunga juhudi za kujenga familia bora na Taifa imara ,shirika hilo linashirikiana na Serikali katika kutekeleza mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Katika maeneo 8 (thematic areas) sisi tunatekeleza 6 na timu ya Wizara imeshafika Mkoani Shinyanga zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti wakaenda mpaka vijijini kabisa kukutana na wananchi na kuona jinsi tunavyotekeleza mpango huu kwa vitendo na matokeo yanayopatina. “ameeleza Bw.Sokoine