Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DK.Tulia Ackson ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas,akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere,akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka Kwenye uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
SEHEMU ya washiriki wakifatilia uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi kwa naiba ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka Kwenye uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika uzinduzi wa filamu ya The Tanzania Royal Tour katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma,Mei 15, 2022. Kutoka kushoto ni Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda.
……………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waunge mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza kwa bidii filamu ya Royal Tour pamoja na vivutio mbalimbali vilivyoko nchini.
“Ninawasihi Watanzania tusishawishike kudharau vya kwetu, tusimame pamoja kutangaza vivutio vyetu na kupitia utalii huu, tutafungua ajira kwa waongoza utalii na kada nyinginezo,” amesema.
Ametoa wito huo leo usiku (Jumapili, Mei 15, 2022) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma waliofika kushuhudia uzinduzi wa filamu hiyo, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
“Baada ya hapa, wana Dodoma twende tukaisemee filamu hii kwa kutumia simu zetu na mitandao ya kijamii,” amesema Waziri Mkuu ambaye alikuwa akimwakilisha Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Amesema kuzinduliwa kwa filamu ya Royal Tour kumefungua zaidi milango ya utalii na kwani baada tu ya uzinduzi Tanzania ilipokea watalii 796 kutoka Israeli ambao walikuja kwa ndege tatu zilizofuatana.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka Wakuu wengine wa Mikoa watenge siku moja na kuwashirikisha wananchi wao washuhudie kazi kubwa ambayo imefanywa na Mheshimiwa Rais.
“Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Mtaka yeye kaanza. Ni vema Wakuu wengine wa Mikoa watafute siku moja ya kuwaonesha watu wao, wanaweza kuchagua hata kwenye ngazi ya Halmashauri ili waone juhudi za Mheshimiwa Rais wetu,” amesisitiza.
Amesema kitendo cha Mheshimiwa Rais Samia kuruka kwa ndege na kuonesha kwa karibu kilele cha Mlima Kilimanjaro, kimekata mzizi wa fitna juu ya mahali halisi ulipo mlima huo. “Mheshimiwa Rais amekata mzizi wa fitina na kuithibitishia dunia kuwa Mlima Kilimanjaro uko Tanzania.”
Akielezea fursa zilizopo kwenye mkoa wa Dodoma, Waziri Mkuu ametaja kilimo cha zabibu, usindikaji wa mvinyo, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), eneo la kuandaa wapigania uhuru wa Namibia, Angola, Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji, mapori ya akiba ya wanyamapori ya Mkungunero na Swagaswaga na mazalio ya wanyama ya hifadhi ya Tarangire kama baadhi ya vitu vinavyoweza kuuinua mkoa huo.
“Uendelezaji wa vivutio hivi utawafanya wakazi wa Dodoma wapate mahali pa kupumzikia, nawasihi wawekezaji waje Dodoma sababu ni mahali sahihi kwa uwekezaji na utalii.”
“Si hivyo tu, fimbo ya Mtemi Mazengo iko Dodoma, baiskeli yake aliyotumia iko Dodoma, kaburi lake liko Dodoma na pia nyumba ya kuhifadhi madini iliyojengwa mwaka 1925. Ninatoa wito kwa Bodi ya Utalii ishirikiane na uongozi wa Mkoa wa Dodoma ili kuhifadhi vivutio hivi.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas alisema matarajio ya awali yalikuwa kuwafikia watu bilioni moja lakini kutokana na tafiti za kisasa, matarajio ya sasa ni kuwafikia watu bilioni mbili.
Alisema filamu ya Royal Tour ni fursa ya pekee ya kuitangaza Tanzania, ni fursa ya kutandaa duniani (networking) kwani imemuwezesha Mheshimiwa Rais kukutana na wafanyabiashara maarufu na wamiliki maarufu wa makampuni makubwa duniani ya utalii, filamu, meli za utalii na mahoteli maarufu.
Naye,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema serikali ya mkoa wa Dodoma ina nafasi kubwa katika kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa mkoa wa utalii nchini.
Mtaka amesema Mkoa wa Dodoma una sehemu mbalimbali za utalii ikiwemo utalii wa michoro ya mapango Kondoa , Dodoma ,utalii wa Zabibu.
Aidha,Mtaka amesema ,katika mkoa wa Dodoma una utalii wa miradi mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za mkoa.
“Dodoma tuna utalii wa miradi,tunatamani kila mtanzania apate fursa ya kuwekeza katika mkoa wa Dodoma ,tutahakikisha tunachepusha sekta binafsi mkoa wa Dodoma,na kuhakikisha unakuwa mkoa kila mfanyabiashara ananufaika na makao makuu ya nchi”amesema.
Kuhusu utalii wa mikutano Mkuu huyo wa mkoa amesema sasa mkoa wa Dodoma una una sehemu mbalimbali ya mikutano hivyo imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa sekta binafsi.
“Tunahamasisha utalii wa mikutano,watu waone ni fursa kubwa katika mkoa wa Dodoma ,Dodoma ni mji wa serikali itapendeza Zaidi katika kusaidia na kuchochea ukuaji wa sekta binafsi.
Uzinduzi wa Royal Tour Mkoa wa Dodoma umezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa kwa niaba ya Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere,Waziri wa Maliasili na Utalii,Pindi Chana,Spika wabunge Dkt.Tulia Ackson ,wananchi na wafanyabiashara mkoa wa Dodoma ambapo unarushwa mbashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Ikumbukwe Uzinduzi wa Royal Tour ulizinduliwa na Rais Samia katika Mikoa ya Arusha,Zanzibar,Dar es Salaam na leo umezinduliwa Mkoa wa Dodoma.