Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Furahika Education Bw. Tambula Mabula akizungumza jambo katika Mahafali Tisa ya Chuo hicho yaliofanyika tarehe 13/5/2022 jijini Dar es Salaam.
aimu Mkurugenzi wa Chuo cha Furahika Education Dkt. David Msuya akizungumza jambo katika Mahafali Tisa ya Chuo hicho yaliofanyika tarehe 13/5/2022 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Furahika Education wakiwa katika picha ya pamoja katika Mahafali ya Tisa ya Chuo hicho yaliofanyika tarehe 13/5/2022 jijini Dar es Salaam.
………………………………..
Zaidi ya Wahitimu 58 Chuo Furahika Education Tanzania mwaka 2022 wametakiwa kutumia ujuzi walioupata kwa kujiajiri pamoja na kufanya kazi kwa kubidii jambo ambalo litawasaidia kupiga hatua katika nyanja mbalimbali kimaendeleo na kupata mafanikio katika maisha yao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo tarehe 13/5/2022 katika ya Mahafali Tisa ya Chuo cha Furahika Education Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Furahika Bw. Tambula Mabula, amewataka wahitimu kutumia elimu walioipata kwenda kujiajiri na kuondokane na dhana ya kuletewa ajira bali wajitume ili waweze kufanikiwa kiuchumi.
Bw. Mabula ni mgeni rasmi katika mahafali hayo, ambapo ameeleza kuwa siri ya mafanikio katika maisha ni kufanya kazi kwa bidii, huku akiwasisitiza wahitimu wanapaswa kuwa mabalozi wazuri katika sehemu mbalimbali watakapopata fursa ya kufanya kazi.
“Bodi ya Chuo ina malengo kuweka kozi mbalimbali jambo ambalo litasaidia vijana kupata elimu ambayo itakuwa msaada katika maisha yao na familia kwa ujumla” amesema Bw. Mabula.
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Furahika Education Dkt. David Msuya, amewapongeza wahitimu wote kwa kumaliza salama masomo yao na kuwataka kwenda kujituma kwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Dkt. Msuya amesema kuwa katika mahafali hayo kuna wahitimu zaidi ya 58 wamefanikiwa kupata mafunzo ngazi ya cheti katika fani mbalimbali ikiwemo ya Computer, Mapambo na Mekapu, Hotel Management, Secretarial pamoja na Ufundi wa kushona.
Ametoa wito kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao katika kipindi chote na masomo na baada ya kumaliza ili kuhakikisha wanapata sehemu rafiki ya kufanyia kazi.
“Wazazi mnapaswa kuwa utamaduni wa kuwafatilia watoto wenu muda wote wakiwa chuoni kwa sababu kuna baadhi ya wanafunzi ni wazembe hawafiki darasani jambo ambalo linaleta usumbufu kwa maendeleo yake” amesema Dkt. Msuya.
Amesema kuwa Chuo cha Furahika wanafunzi wanasoma bila kulipa ada, lakini wazazi wanachangia gharama ndogo za mithiani pamoja vitendea kazi (material) kwa ajili ya mafunzo kwa njia ya vitendo.
Katika hatua nyengine Dkt. Msuya ametangaza kozi mpya ya Uuguzi (Nursing) ambapo ameeleza kuwa mwisho wa kutuma maombi ya kujiunga na kozi hiyo Mei 16 mwaka huu, na mwezi mei 18, 2022 masomo ya kozi hiyo yanatarajia kuanza.
Amefafanua kuwa kozi ya uuguzi imefadhiliwa na wafadhili kutoka nchini Marekani kupitia Mradi wa Msaidie Mama Mjamzito ambayo itatolewa kwa muda wa mwaka mmoja na wahitimu watakwenda kufanya kazi katika vijiji mbalimbali katika Mikao ya Tanzania.
“Mradi wa Msaidie Mama Mjamzito umelenga kuisaidia serikali katika kutoa huduma katika sekta ya afya kwa maendeleo ya taifa, na sifa ya kujiunga na kozi ya uunguzi mwanafunzi anatakiwa kuwa na alama D katika somo la biology ” amesema Dkt. Msuya.
Chuo cha Furahika Education kimesajili na VETA na wanatoa kozi mbalimbali bure bila kulipa ada, hivyo wananfunzi wanachangia ada ya mitihani wanayofanya ili aweze kupata cheti.
Lengo la Chuo ni kuendeleza watoto wa kike na vijana kuwapa ujuzi mbalimbali kwaajili ya mafanikio yao na familia kwa ujumla.