Home Mchanganyiko TANZANFRIKA TOURISM GROWTH YAZITAKA TAASISI ZA MAZINGIRA KUZINGATIA UFANYAJI USAFI KWENYE MAENEO...

TANZANFRIKA TOURISM GROWTH YAZITAKA TAASISI ZA MAZINGIRA KUZINGATIA UFANYAJI USAFI KWENYE MAENEO YA MIJI

0

*********************

Taasisi za serikali na binafsi zinazojihusisha na masuala ya mazingira zimeombwa kuweka ushirikiano katika zoezi la kuweka safi maeneo mbalimbali yanayosahaulika ikiwemo fukwe za bahari

Ombi hilo limetolewa leo Mei 14,2022 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya TanzanAfrika Tourism Growth, Bi.Jachrine Leonard, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi lililofanyika katika fukwe za bahari maeneo ya hosptali ya Agakhan kata ya Kivukoni liliratibiwa na taasisi yake inayojihusisha na kutangaza vivutio vya utalii na kutunza mazingira.

Aidha Bi.Jachrine ameziomba taasisi hizo kuunga mkono juhudi zao kwa kushirikiana katika shughuli hizo huku akidai kuwa zoezi hilo litakuwa ni mwendelezo wa kufanya usafi maeneo mbalimbali ili kuweza kuweka mazingira safi salama ili kuvutia watu kutalii maeneo ya vivutio.

Kwa upande wake mtendaji wa mtaa wa huo, Ashura bwatamo ameziomba serikali na wadau muhimu kujitokeza kuwasaidia vifaa kwani wanakabiliwa na changamoto ya uchache wa vifaa vya usafi.