Sehemu ya washiriki wa siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa LUPUS TANZANIA iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es salaam tarehe 14 Mei 2022.
Sehemu ya washiriki wa siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa LUPUS TANZANIA iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es salaam tarehe 14 Mei 2022.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Afolf Mkenda
amesema kuwa serikali imedhamiria kuwekeza zaidi kwenye elimu ya utafiti na
tiba.
Huo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
ya mwaka 2020-2025 na mpango mkakati wa serikali kupitia bajeti ya Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2022/2023 ambapo imepanga kutoa motisha kwa
wahadhiri kutoka chuo chochote cha serikali ama binafsi akiweza kuchapisha
andiko lake kwenye majarida ya juu, serikali itampa Shilingi milioni hamsini.
Waziri Mkenda ameyasema hayo tarehe 14 Mei 2022 wakati wa siku
ya maadhimisho ya ugonjwa wa LUPUS TANZANIA iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es salaam.
Waziri Mkenda mesema kuwa kwa jumla yake serikali imetenga
Bilioni moja kwa ajili ya wahadhiri hao na kufanya hivyo serikali inalenga
kujenga uhusiano na uwezo zaidi kwa watafiti ili kuimarisha kipato chao jambo
litakalowafanya waweze kufanya utafiti wakati wote na kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Amesema kuwa serikali itawawezesha wanafunzi wote ikiwemo
kuwasomesha katika vyuo vikuu kwa wale watakaofaulu kwa kiwango cha juu kwenye
masomo ya Sayansi.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Andrea Pembe
amesema kuwa serikali imeweka kipaumbele kwenye magonjwa mbalimbali ikiwemo
uraibu wa madawa ya kulevya na magonjwa ya kina mama yatokanayo na ujauzito
hivyo kuwepo kwa huduma hiyo nchini kumerahisisha kuwahudumia wananchi kwa
kuwapatia tiba kirahisi wagonjwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji kwa urahisi wa
dawa japo gharama za dawa bado ni kubwa sana.
Prof Pembe amesema kuwa katika tafiti zilizofanyika kwenye
ugonjwa wa Lupus zinaonyesha watu wa asili ya Afrika ndio waathirika wakubwa na
inakadiriwa watu 70-100 wanaathirika na ugonjwa wa Lupus kati ya watu 100,000.
Waziri Mkenda ameongeza kuwa wanawake ndio wanaathirika zaidi na
ugonjwa huo kwa uwiano wa wanawake 10 kwa mwanaume mmoja.
Aidha katika utafiti uliofanyika katika hospitali ya Taifa
kutambua watoto waliokuwa na magonjwa rheumatism kwa kipindi cha miaka 7
(2012-2019) ulitambua watoto 52 waliokuwa na hayo magonjwa na miongoni mwao
watoo 8 ambao ni sawa na asilimia 15% walikuwana ugonjwa wa Lupus.