Meneja wa maabara ya chakula na dawa kutoka Mamlaka ya maabara
ya Mkemia mkuu wa Serikali Dkt. Shimo Peter wakati akizungumza na waganga wa
tiba asili kwenye warsha ya wadau wa tiba asili na tiba mbadala kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania.
Mkuu wa Mradi wa GRILL na VaSHPARD kutoka SUA Dkt. Faitha Mabiki amesema lengo la warsha hiyo.
Mkemia Dkt. Richard Madege akitoa matokeo ya majibu ya vipimo vya dawa zilizopimwa katika maabara ya SUA kuangalia ubora wa dawa hizo zinazozalishwa na waganga wa tiba asili.
Prof. Robinson Mdegela akifundisha kuhusu madhara ya vimelea tajwa kwa afya ya binadamu na akifafanua matokeo ya utafiti ya sampuli hizo za dawa kwa ujumla wake.
KATIKA kuhakikisha
Wagaga wengi wa tiba asili nchini wanauza dawa bora na salama kwa
binadamu,Wanyama na mazingira Mkemia Mkuu wa Serikali amepunguza gharama
za upimaji wa dawa hizo ili zipimwe na kusajiliwa kisheria.
Hayo yamebainishwa
na Meneja wa maabara ya chakula na dawa kutoka Mamlaka ya maabara ya Mkemia
mkuu wa Serikali Dkt. Shimo Peter wakati akizungumza na waganga wa tiba asili
kwenye warsha ya wadau wa tiba asili na tiba mbadala kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania iliyoratibiwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia mradi wake
wa VaSPHAD.
“Kumekuwa na maombi
ya muda mrefu ya waganga wa tiba asili kuomba Mkemia Mkuu wa Serikali kupunguza
gharama za upimaji wa dawa ili waweze kusajiliwa kwahiyo mkemia mkuu
ameliangalia na hatimae amepunguza gharama kutoka dola za kimarekani 311 hadi
kufikia dola 152 ambayo ni karibu nusu ya gharama za awali” alisema Dkt. Shimo.
Amefafanua kuwa ili
kuweza kupimiwa kwa kutumia punguzo hilo kuna taratibu ambazo wanapaswa
kuzifuta Waganga hao ambayo ni kujaza fomu kutoka baraza la tiba asili na tiba
mbadala au waratibu wa wa tiba asili kutoka wilayani au mkoani na kwamba
kinyume na hapo watajikuta wanalipa zaidi ya dola 500 kwa dawa moja.
Amewataka kufikisha
taarifa hizo kwa wenzao kote nchini ili waweze kutumia fursa hiyo walioyoiomba
kwa muda mrefu mara kwa mara iliyotolea na Mkemia Mkuu wa Serikali ili waweze
kuuza dawa zenye viwango na ubora utakaowawezesha kufikia soko la ndani na la
nje ya nchi.
Amewasisitiza watoa
huduma kuzalisha dawa asili kufuata kanuni na miongozi ya uzalishaji bora na
salama kutumia kemikali kufuata sharia ya kemikali namba 3,2003 inayosimamiwa
na GCLA na kupata mafunzo ili kuweza kutambua njia salama za matumizi ya
kemikali.
Awali Mkuu wa Mradi
wa GRILL na VaSHPARD kutoka SUA Dkt. Faitha Mabiki amesema lengo la warsha hiyo
ni kuedeleza jitihada za Chuo na Serikali katika kubadili tabia za namna
wanavyotengenza dawa za asili na wanavyotoa huduma kwa jamii.
“Kwa kuwa toka
tumeanza mradi tumeona mabadiliko makubwa sana katika utengenezaji wenu wa dawa
na utoaji wenu huduma hivyo tunaamini warsha kama hii inayowakusanyisha pamoja
kutoka mikoa mbalimbali na kupata mafunzo kutawasaidia zaidi kutoka kwenye
kufanya kazi kwa mazoea kwa kubadili tabia na hatimae kutengeneza dawa asili
zenye viwango vinavyokubalika katika soko la ndani na nje ya nchi”alieleza Dkt.
Mabiki.
Mtafiti huyo
amesema kwenye warsha hiyo pia watatoa matokeo ya vipimo vya dawa zao
mbalimbali walizozipeleka SUA kwaajili ya vipimo zilizobaki kutoka kwa
Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye aliomba wataalamu wa SUA kusaidia kuzipima
na kuwapatia majibu kila mmoja na kumshauri mambo ya kufanya ili kufikia ubora
unaotakiwa.
Amesema dawa kutoka
nje ya nchi tunazoziona zinapitia michakato mingi ili kuweza kupata nembo za
ubora na mamlaka za nchi hizo na kimataifa ndio maana SUA na Serikali kupitia
mkemia mkuu wa serikali wanashirikiana ili kuwawezesha waganga hao waweze
kufikia soko kirahisi la nje.
Amewataka kuendelea
kushirikiana miongoni mwao na kuwasiliana katika masuala mbalimbali kwakuwa
kila mmoja ana uelewa tofauti kutokana na mazingira wanayotoka na itawasaidia
kupeana ujuzi na kuongeza uelewa zaidi badala ya kila mmoja kufanya mambo yake
kwa siri.
Akizungumza kwa
niaba ya waganga wengine walioshiriki warsh hiyo Dkt.Flavian Nyakeji kutoka
Njombe amemshaukuru Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kusikia kilio cha cha gharama
kubwa za upimaji wa dawa na kuahidi kuitumia fursa hiyo vyema ili kuweza
kufikia viwango.
“Swala la gharama
kubwa za upiamaji limekuwa kilio chetu cha muda mrefu maana wengi wetu kweli
tunazo dawa za asili znuri na zinatibu lakini hatuna uwezo wa kulipa dola 500
na zaidi kupima dawa moja ili tusaijiliwe lakini sasa kwa gharama hiyo ya
shilingi dola 152 tutahakikisha tunapima dawa zetu kwa faida yetu,jamii
na wateja wetu” alisema Dkt.Nyakeji.
Katika warsha hiyo
mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo,aina za vioungo vya kemikali kwenye
mimea,Utengenezaji wa kemikali,kazi za kemikali kwenye mimea na utabibu,athari
za sumu kuvu katika afya na biashara,namna ya kupunguza na kuzuia sumu kuvu
kwenye kwenye bidhaa,Matatizo ya kiafya yanayosababishwa na vimelea, mambo
hatari yanayochangia kuwepo kwa vimelea pamoja na mada zingine nyingi.
Warsha hiyo
imewakutanisha waganga wa tiba asili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
hususani wale ambao walipeleka dawa zao kwa mkemia mkuu wa serikali kwaajili ya
vipimo na zikabaki ili waweze kupewa majibu ya dawa zao.