Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea cheti cha ithibiti ya utoaji wa huduma za uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof.Othman Chande Othman,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea cheti cha ithibiti ya utoaji wa huduma za uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa SADCAS,Bw. Victor Mundembe,akitoa salaam kutoka SADCAS wakati wa hafla ya kupokea cheti cha ithibiti ya utoaji wa huduma za uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga,akielezea historia fupi ya tbs CB na utendaji kazi wake wakati wa hafla ya kupokea cheti cha ithibiti ya utoaji wa huduma za uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kupokea cheti cha ithibiti ya utoaji wa huduma za uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe,akipokea cheti cha kimataifa cha ithibati cha utoaji huduma uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa SADCAS,Bw. Victor Mundembe.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof.Othman Chande Othman,hafla iliyofanyika leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe,akimkabidhi cheti cha kimataifa cha ithibati cha utoaji huduma uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kilichotolewa na Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof.Othman Chande Othman.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt.Athuman Ngenya hafla iliyofanyika leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt.Athuman Ngenya,akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe (hayupo pichani) mara baada ya kuongoza zoezi la kupokea cheti cha ithibiti ya utoaji wa huduma za uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuongoza zoezi la kupokea cheti cha ithibiti ya utoaji wa huduma za uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma.
…………………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS),limepokea cheti cha kimataifa cha ithibati cha utoaji huduma uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti huku Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe ameipongeza TBS kwa hatua hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea cheti hicho kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma,Naibu Waziri Kigahe amesema huo ni uthibitisho na ushuhuda tosha kuwa TBS inaendelea kujizatiti na kutambulika kimataifa kupitia utekelezaji wa majukumu yake.
Kigahe amesema kuwa ithibati ina manufaa makubwa kwa taasisi za umma na binafsi na TBS inatoa huduma kwa gharama nafuu ikilinganishwa na gharama zinazotozwa na kampuni za nje ambazo zimekuwa zikitoa huduma hizo.
“Niwapongeze TBS kwa kufikia hatua hii kubwa ya kupata ithibati ya umahiri katika kutoa huduma ya ithibati ya umahiri katika kutoa huduma hii, sina shaka mtaendelea kudumisha na kuongeza wigo kwenye kutoa huduma zenye ithibati ya umahiri ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa,”amesema Mhe.Kigahe
Aidha amesema kuwa hivi karibuni,makampuni ya nje yalipata changamoto kutokana na janga la UVIKO-19 hivyo kushindwa kutoa huduma kwa wateja wao,hali iliyopelekea wateja wao kupoteza uhalali wa kuwa na vyeti vya uthibitisho wa mifumo ya kimenejimenti.
”kutokana na tatizo hilo baadhi ya taasisi tayari zimefanya uhamisho wa kupata huduma ya uthibitisho wa mifumo ya kimenejimenti kutoka kampuni za nje kwenda TBS ili kunufaika na huduma ya uhakika kwa gharama nafuu.”amesema
Hata hivyo ametoa wito kwa taasisi za umma na sekta binafsi kuthibitisha mifumo yao ya kimenejimenti kwa kuitumia TBS ambayo imepokea cheti cha Kimataifa cha ithibati katika huduma hii.
”Tutaendelea kuisaidia TBS katika kutimiza majukumu yake na kuhakikisha inaendelea kuwahudumia wananchi kwa umahiri na ufanisi katika nyanja zote za uzalishaji bidhaa na utoaji huduma kwa mujibu wa sheria ya viwango Na.2 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake”amesema Naibu Waziri
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga, ametaja hatua mbalimbali za kupata cheti hicho kuwa ni pamoja na kuweka na kufuata mifumo kulingana na matakwa yaliyoainishwa kwenye kiwango cha kimataifa ISO/IEC 17021.
“Kujipima utendaji kwa mujibu wa kiwango husika pamoja na matakwa ya tume ya ithibati na kuwa na wataalam wenye umahiri na weledi katika dhana nzima ya utoaji huduma,”amesema Bw.Msasalaga
Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa SADCAS,Bw. Victor Mundembe,ameitaka TBS kuhakikisha inazingatia ubora kwenye utoaji huduma hizo ili viwango vya ithibati hiyo visishuke.
Naye Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt.Athuman Ngenya amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuwatangazia wananchi, taasisi za umma na sekta binafsi kuwa huduma hiyo kwa sasa ipo TBS.