Na Mwandishi wetu, Mirerani
OFISA Madini mkazi (RMO) wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Fabian Mshai anatarajiwa kukutana na wachimbaji madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani leo alhamisi ya Mei 12.
RMO Mshai anatarajiwa kukutana na wamiliki ambao ni wachimbaji madini, mameneja wa migodi kwenye ukumbi wa Kazamoyo Inn kwa Diwani Luka.
Amesema lengo la mkutano huo ni kukutana na wachimbaji hao na kusikiliza changamoto zinazowakabili kwenye shughuli zao za uchimbaji wa madini.
“Tutakutana na wachimbaji madini na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuona namna ya kuzitatua,” amesema RMO Mshai.
Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Justin Nyari amesema wachimbaji madini wanapaswa kuhudhuria kwa wingi ili waweze kuzungumzia changamoto zinazowakabili.
“Tunatarajia wachimbaji madini watahudhuria kwa wingi kwa ajili ya mkutano huo ili wazungumze na RMO Mshai,” amesema Nyari.
Mmoja kati ya wamiliki wa mgodi kwenye machimbo ya kitalu D, Theresia Wapalila amesema wachimbaji hao wanapaswa kuandikiwa barua kwenye kila mgodi Ili waweze kuhudhuria kwa wingi.