Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akiwa na Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu nchini Walece Karia kwenye mkutano wa itifaki ya maandalizi ya mkutano wa Shirikisho la mpira wa Miguu barani Afrika CAF utakaofanyika mkoani Arusha Mwezi wa nane mwaka huu picha zote na Prisca Libaga Maelezo Arusha.
…………………………………………………
Na Prisca Libaga Maelezo Arusha
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia amefanya mkutano na Uongozi wa Mkoa wa Arusha juu ya maandalizi ya kufanyika kwa mkutano mkuu shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika CAF.
Mkutano huo utafanyika hapa nchini mapema ifikapo mwezi wa nane Mkoa Arusha, huku viongozi wa mashirikisho ya mpira wa miguu Afrika wakitajwa kuhudhuria Mkutano huo, wachezaji wa zamani wa mpira wa miguu Afrika pamoja na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) Gianni Infantino
Kupitia hilo Rais Karia amesema watatumia Fursa hiyo kufanya utalii wa kimichezo pamoja na utalii wa kimikutano lengo likiwa kuunga mkono juhudi za Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii wa ndani huku Serikali ya Mkoa wa Arusha ikiwa katika hali nzuri ya maandalizi hayo
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema wananchi wa mkoa huo wajipange sawa sawa na fursa ya mkutano huo ili kuendeleza maendeleo ya michezo na kiuchumi kwa mkoa wetu.
Amebainisha kwamba mkutano huo utaenda kuleta chachu ya maendeleo kama mkoa tutajipanga kisawa sawa kufanikisha mkutano huo mkubwa ambao umekuja Wakati wa msimu mkubwa wa Utalii nchini.