Mkuu wa Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzania ACP Issack Katamiti akizungumza wakati wa operesheni maalum ya kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzania ACP Issack Katamiti akisisitiza jambo wakati wa operesheni maalum ya kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzania ACP Issack Katamiti akionesho moja ya leseni ya kibari ya kampuni binafsi ya ulinzi wakati wa operesheni maalum ya kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Meneja msaidizi Mamlaka ya Mapato ( TRA) Dodoma Bw. Silver Rutagwelera akizungumza wakati wa operesheni maalum ya kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Msimamizi na Mwandikishaji Wanachama NSSF, Bw.Hussein Dotto akizungumza wakati wa operesheni maalum ya kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Mratibu wa Mfumo wa Kusimamia Sekta Binafsi ya Ulinzi Tanzania (PSGP), Bw.Macmillan George akizungumza wakati wa operesheni maalum ya kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***************************
Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzania limesema halitasita kuyachukulia hatua kali za Kisheria Makampuni yote ya ulinzi Binafsi yenye mapungufu yanayotakiwa kisheria.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati operesheni maalum kuyakagua na kufuatilia mienendo ya ufanyaji kazi wa makampuni binafsi ya ulinzi yaliyopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni operesheni endelevu kukagua katika makampuni hayo.
Akizungumza katika operesheni hiyo Mkuu wa Dawati la Makampuni Binafsi ya Ulinzi na Polisi Wasaidizi Tanzani ACP Issack Katamiti amesema kuwa kama watabaini kuwa kuna makampuni hayafuati sheria, taratibu na kanuni na miongozo inayotakiwa ambayo miongozo inatolewa na Mamlaka za serikali, watayafutia kibari.
“Inawezekana kabisa yappo makampuni ambayo hayafuati utaratibu uliopo ikiwemo kutokulipa kodi (TRA), mikataba inasusua kwa wafanyakazi na hata wengine wamekuwa hawapo nadhifu kwenye mavazi kupitia wafanyakazi wao”. Amesema ACP Katamiti.
Kwa upande wake Meneja msaidizi Mamlaka ya Mapato ( TRA) Dodoma Bw.Silver Rutagwelera amezitaka kampuni zote binafsi za ulinzi kutunza kumbukumbu zao zote kitendo kinachopelekea kutambulika kwa urahisi utendaji kazi wao.
“Tunaangalia makadirio na mapato, uwasilishaji wa return za mwezi au mwaka,mikataba ya malindo na jengo,paylow, mishahara ya wafanyakazi ili kuweza kubaini kama kodi inayokatwa na kuwasilishwa kwetu pamoja na mengine yanayoweza jitokeza” alisema Rutagwelera
Naye Alice Milanzi kutoka Idara ya Kazi mkoa wa Kazi Temeke amesema kuwa wamekuwa wakiangalia mambo mbalimbali ikiwemo stahiki zao mbalimbali kwa kujibu wa sheria ikiwemo ikiwemo mikataba ya kazi, paylow ili kujiridhisha kama wafanyakazi wanalipwa sawa kulingana na kazi wanayofanya.
Katika hatua nyingine msimamizi wa uandikaji kutoka mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF), Hassan Dotto amesema kuwa wamekuwa wakifuatilia mishahara inayolipwa kama inaendana na kinachowasilishwa katika mfuko huo.
Imeelezwa kuwa waajiri wote na waajiriwa wa kampuni za ulinzi wametakitakiwa kuhakikisha kuwa wameungwa katika mfumo wa PSGB.