Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( SUZA) Prof. Mohammed Makame akizungumza katika kongamano la kuadhimisha siku ya wauguzi Duniani lililoandaliwa na wanafunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Mbweni, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakunga na wauguzi Zanzibar Prof.Amina Abdul-qadir Ali . Mwakilishi Kutoka jumuiya ya kusaidia wagonjwa wasiojiweza na wasio na jamaa (JAI ) Ustadh Amir Shaib akiwasilisha mada ya umuhimu wa Imani na huruma ya wauguzi Kwa wagonjwa , wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya wauguzi Duniani lililoandaliwa na wanafunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Mbweni ,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mwanafunzi kutoka Zanzibar University (ZU) Kada ya uuguzi na Ukunga Muumin Idrisa Kai akichangia mada wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya wauguzi Duniani lililoandaliwa na Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Mbweni, huko Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR
*****************************
Na Rahma Khamis- Maelezo Zanzibar 12/5/2022
Wauguzi na Wakunga wametakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa wagonjwa wanaofika katika vituo vya afya ili kuepusha malalamiko pindi wanapohitaji kupatiwa huduma hizo.
Akizungumza na wanafunzi wa afya katika kongamano la kuadhimisha siku ya wauuguzi duniani Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Prof, Mohd Makame katika Ukumbi Shekh Idrissa Abdulwakili Kikwajuni amesema kazi ya uuguzi na ukunga ni kazi ngumu hivyo inahitaji imani na huruma katika kutekeleza majukumu yao.
Amesema maadhimisho ya siku hiyo ni muhumu kwa wauguzi na wanakunga kwani inakumbusha mambo mbalimbali yanayohusu afya za wanadamu wajibu wa wahudumu wa afya kufanya kazi kwa kwa kujituma ili kuimarisha afya za wananchi.
Aidha Prof Makame amefahamisha kuwa Serikali inathamini michango ya wauguzi na wakunga katika kutengeneza kada hiyo na kuifanya kuwa ya kutegemewa na wananchi kwa kusaidia kutatua matatizo yanayoihusu jamii.
Pia ameeleza kuwa kuadhimisha siku hiyo inaenda sawa na mikakati ya dunia katika kuekeza kitaaluma kutokana na wanafunzi kujiunga katika vyuo mbalimbali ili kuipata taaluma hiyo na kuifanyia kazi.
Hata hivyo amewaasa wanafunzi kuendelea kujiongeza kielimu Zaidi na kufanya kazi kwa bidi ili kutoa huduma bora katka jamii na kuahidi kuzifikisha sehemu husika changamoto zinazowakabili wauguzi na wakunga ili ziweze kufanyiwa kazi.
Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wauguzi na Zanzibar Prof, Amina Abdulkadir Ali na Kaimu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Dr. Rukia Rajab wameiomba Serikali kupitia W izara ya Afya kuwapatia idara ya wauguzi na wakunga katika Skuli yao.
Aidha wamefahamisha kuwa katika kuimarisha huduma za afya nchini Wizara imeunda Idara ya Uguzi na Ukunga kwa lengo la kuwapatia huduma Zaidi wagonjwa ili na wao wajisikie katka hali nzuri. hivyo na wao wanaomba kupatiwa
Sambamba na hayo wamewahimiza wauguzi na wakunga kuhakikisha kuwa kila mgonjwa wanaemuhudumia kufurahishwa na huduma wanazopatiwa.
Siku ya wauguzi na wakunga duniani huwadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 12/5 ambapo kauli mbiu yam waka huu WAUGUZI SAUTI INAYOONGOZA, WEKEZA KWENYE UUGUZI NA HESHIMU HAKI KULINDA AFYA KWA WOTE.
Kongamano hilo limmeandaliwa na wanafunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba na kuwashirikisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo Skuli ya afya Mbweni,Skuli ya afya kwa Mchina na Military Collage Medical Science kampas ya Bububu pamoja na Zanzibar University.