**********************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKURUGENZI wa kiwanda cha Animal Care co.Ltd , Mlandizi,Kibaha Mkoani Pwani ,Dkt Salaa Hamdun amesema endapo Serikali itaendelea kutatua changamoto ya wafugaji katika usimamizi wa kupata soko la uhakika kwenye maziwa na bidhaa za mifugo pamoja na kuweka Bei elekezi itasaidia kuongeza kipato Chao.
Akizungumza namna wanavyosaidiana na jamii inayowazunguka na Wafugaji , Mkurugenzi wa kiwanda hicho kinachozalisha vyakula vya mifugo na virutubisho alisema, bei bado ni ndogo kwa bidhaa za mifugo ukilinganisha na Gharama za vyakula ambazo zinapanda huku bei ya kuku sokoni ikiendelea kumbana mfugaji na mkulima moja kwa moja.
“Suala Kama Hilo Ni kusema Serikali isaidie wafugaji kuweza kusimamia masoko Yao na kucontrol bei maana bei ya maziwa , bidhaa za mifugo bado ndogo”;”; alifafanua Hamdun.
Hamdun alieleza kwamba, kiukweli wafugaji wanapata Faida ndogo na wakati mwingine kupata hasara kubwa hivyo sekta ya kilimo kupitia Serikali ni vyema ikatupia macho suala hili ili kupunguza makali ya kimaisha kwa kundi la wafugaji.
Vilevile alishukuru Serikali kwa kuendelea kusimamia wawekezaji na changamoto zinazowakabili hasa kutatua kero ya umeme,maji na baadhi ya miundombinu.
Alisema,kiwanda cha Animal Care sasa kinazalisha vyakula vya mifugo na virutubisho Tani 2,500 kwa mwezi na kutoa ajira 200 za moja kwa moja.
Hamdun alielezea , wanatumia malighafi za kitanzania kwa asilimia 90,”Tuna mchango ndani ya jamii inayotuzunguka ,na jamii, wafugaji wanamchango kwetu tukiwa kama wawekezaji.
Alisema, licha ya hayo Lakini malighafi nyingine kama soya,mahindi wanapata Zambia na Malawi Jambo ambalo ni changamoto kwao.
Aliomba wafugaji kukimbilia fursa ya kutumia kiwanda hicho kurahisisha kupata soko huku changamoto zao zikiendelea kufanyiwa kazi.
Awali mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri,alisema wilaya inaendelea kushirikiana na wawekezaji pamoja na wafugaji kutatua changamoto zinazowakabili ili kuinua maendeleo ya sekta ya Mifugo na kukuza uchumi.
Kiwanda hicho Ni moja ya viwanda ambavyo vimetembelewa na mwenge wa uhuru Mkoani Pwani na kuhimiza wawekezaji kutoa ajira hasa kwa wazawa , kushirikiana kwa maendeleo ndani ya jamii na kulipa Kodi ili kuongeza Pato la Taifa.